Kabla Hujalipwa... Jiulize Kwanza!
Tatizo siyo kwamba una kitu unafanya au kuna kazi unazifanya…
Naam, hilo siyo tatizo. Lakini tatizo ni matokeo ya hiyo kazi unayoifanya!
Mara nyingi nimekuwa nikiomba kwa Mungu mwenye vyote, ili kile ninachokifanya kama kazi kidumishe amani ya yake, kifanyike kwa taratibu zake, huku kikileta athari chanya kwenye dunia tunamoishi - ndanimo!
Ndio maana leo nasema na wewe ambaye upo tayari kufanya kila jambo ilimradi ulipwe mshahara au upate kipato...
Kaa chini ujiulize:
“Je, kazi yangu inathamini utu au inaharibu utu wa wengine?”
Ninajua upo mtu ambaye unafundisha watu lakini unawafunga fahamu zao zisizinduke.
Umewageuza watoto wa watu kuwa mifugo, huku wewe unajipatia faida. Hili ni tatizo kubwa! Kwa sababu unachofanya ni kuharibu kizazi cha sasa hadi kijacho.
Urithi mzuri sio mali tu - bali ni elimu ya kuishi kiutu!
Lakini si kila elimu inayofundishwa leo ni ya kiutu - nyingine ni elimu za viumbe waliotokea ulimwenguni wakiwemo: majini, malaika, na roho zisizoeleweka!
Ninajua pia upo mja ambaye umepewa madaraka fulani, lakini yanakutaka upoteze hadi utu wa watoto wa watu - unawapiga virungu, unawaponda kwa marungu, hadi kuwaangamiza! Kwa nini? Kwa sababu ya vihela vya kichimvi?
Naam, unaona umefanikiwa… lakini la hasha! *Umepewa jukumu lisilo la kiutu - linaloondoa utu wa watu huku ukitetea mambo yasiyo ya kiutu!
Kuna mwingine ambaye kazi yake ni kuuza bidhaa haramu - zinazoharibu akili za watu na kuwatoa kwenye mfumo wa kiutu. Naam, pole sana kwa biashara ya kuua roho za watu!
Yupo mwingine ambaye amepewa ofisi, lakini ameigeuza kuwa danguro la hila. Kila anayefika kwake kwa shida, anapigwa bei ya mwili kwanza kabla ya msaada!
Ndugu, sikulaumu. Kwa sababu elimu tuliyorithi haikutufundisha kiutu - ilituondoa kwenye misingi ya kiutu. Kwa hiyo nikupe pole tu wewe mja. Lakini pole isiwe mwisho, amka na ubadilike!
Na kuna mwingine ambaye amegeuza mwili wake kuwa biashara. Anauza mwili wake kama bidhaa sokoni. Sikushangai - mahitaji yakiwa juu, bidhaa hujizua yenyewe.
Lakini basi, wanaume: hizi si zama za kununua vinavyojiuza. Shiriki mijadala yetu ya King Mentorship Program ujue thamani ya kiutu!
Nataka kusemaje?
Nikiwa kijana mdogo niliyejaliwa hekima, nawaambia:
Kabla hujaamua kazi ya kufanya au pa kushikilia ili upate kipato, tafuta kwanza elimu ya kiutu!
Elimu ya kiutu haifundishwi darasani tu. Inaanzia kwenye muujiza wa uumbaji - MTU kuumbwa kwa udongo kutoka mabara yote saba. MTU huyo kwa mujibu wa imani ya JADI ni fumbakasa.
Kisha mwenzake, akaotelea kutoka kwake yaani mwanamke aitwaye Mwasi. Na hapo wakawa Fumbakasa na Mwasi, ambao ndio chimbuko la utu wa watu wote duniani kote!
Sasa kama sisi wote tu sehemu ya vizazi ambavyo vimetokana na hawa wazazi wawili Fumbakasa na Mwasi:
Chuki ya nini?
Virungu vya nini?
Mabomu ya nini?
Uadui wa nini?
Tafuta elimu ya kuishi kiutu. Halafu fanya kazi yoyote kwa kuzingatia utu, hekima, huruma na utii kwa Mungu mwenye vyote!
Wasifu wa Mwandishi
Emmanuel Samuel King’ung’e ni mwanajadi, mlezi wa maadili ya kiutu, na mwanzilishi wa King Mentorship Program.
Ametumia maisha yake kusaidia watu kutambua thamani yao, kujifunza kuishi kwa hekima, na kujinasua kutoka kwenye minyororo ya elimu ya kinyonyaji.
Anaamini kuwa nguvu ya MTU iko kwenye maarifa sahihi, maamuzi yenye hekima, na adabu kwa utu wa wengine.
Kupitia mafundisho yake, ameongoza vijana, wazazi na jamii kuelekea maisha yenye utambuzi, uhuru na ufanisi wa kweli.
Jiunge na King Mentorship Program Leo!
Ikiwa unahitaji maarifa ya kweli kuhusu utu, maisha na mwelekeo sahihi wa mafanikio – basi King Mentorship Program ni kwa ajili yako.
📞 Wasiliana nasi sasa kupitia: 0744284329
🌐 Tembelea: kingmentorshipprogram.blogspot.com
Ndimi: Emmanuel Samuel King’ung’e
Mwanajadi | Mkombozi wa Fikra | Mwalimu wa Maisha | Mtetezi wa Utu
Comments
Post a Comment