KUSUDI: SABABU KUBWA YA KUWEPO KWAKO


Je, umewahi kujiuliza: Kwa nini mimi nipo duniani?

Umewahi kuishi maisha yako ya kila siku huku ndani yako kuna shauku ya kufahamu maana ya uwepo wako?

Kila mtu angalau mara moja hujiuliza maswali haya.

Ndiyo maana, kabla hujaendelea na safari yako ya maisha, ni muhimu kuelewa maana ya KUSUDI.

Sasa hebu tusome kwa makini maelezo yafuatayo kuhusu maana ya kusudi:

Wacha tuangalie maana ya kusudi ili uelewe kile kinachomaanishwa hapa. Nitatoa tafsri kubwa mbili, tafsri ya pili ndiyo itafunga mjadala kuhusu maana halisi ya kusudi. 

Tukianza na tafsri ya kwanza ya kusudi ni ile inayofafanua neno kusudi kama; “kitendo cha kutekeleza mpango wa Mungu kukuumba hapa duniani.” 

Mungu ndiye alifanya maisha yawepo. Kuwepo kwetu sisi watu si kwa sababu ya matakwa yetu wala mapenzi yetu, bali ni kwa sababu Mungu mwenyewe alitaka iwe hivyo. 

Hii ni kusema kwamba, uwepo wa maisha yako hapa duniani ni kwa sababu kuna kusudi lililopo nyuma yake. 

Kwa maana hiyo kuna jukumu maalumu lililopo nyuma ya maisha yako ambalo unatakiwa ulitekeleze. Na katika kuishi kwako huna budi kutekeleza jukumu hilo. 

Lakini swali ni je, unatambua mpango wa Mungu kufanya maisha yawepo? Swali hili litajibiwa ukiwa unaendelea kusoma makala hii! 

Hata ingawa pengine hujajua kusudi lako au hujui kwa nini ulizaliwa, hili halizuii ukweli kwamba kila mtu ameumbwa kwa kusudi fulani. 

Kumbuka, ujinga wa kutokujua kusudi la kitu fulani hauondoi kusudi la kitu hicho. Hivyo basi, ingawa huenda haujui kwa undani kusudi lako, kuna kusudi halisi lililopo nyuma ya maisha yako.

Kwa muktadha huu tunaweza kuhitimisha kutoa tafsiri halisi ya kusudi kama; “ni sababu au lengo kubwa la kuwepo kwa kitu au mtu fulani.” 

Naam hiyo ndiyo maana halisi kuhusu kusudi. Kumbe lipo lengo lililofanya maisha yawepo. Na hilo lengo ndilo kusudi la uwepo wetu. 

Kwa mantiki hiyo tunaweza kusema kusudi, ni mchocheo unaoongoza mafanikio, tabia, na mwelekeo wa maisha yetu. 

Kusudi linajikita katika maono ya juu ambayo hutufanya tuishi kwa maana zaidi ya matumizi ya kila siku. 

Linapohusiana na maisha ya mtu, kusudi si tu kuhusu kufanya kazi au kutimiza matakwa ya kijamii, bali pia ni kuhusu kugundua wapi unakwenda na nini unapaswa kutoa duniani.

Kwa muda mrefu nilikuwa nikitafakari kuhusu chanzo halisi cha uhai - si wa binadamu tu, bali wa kila kiumbe hai tunachokifahamu. 

Nilijiuliza: Kwa nini maisha haya yapo? Kwa nini kila kiumbe kipo? Na je, ni nani aliyesababisha kuwepo kwa huu mfumo mpana unaojiendesha kwa ustadi wa ajabu?

Nilipochunguza kwa kina, nikagundua kuwa kila kiumbe kimeumbwa kwa sababu. Hakuna kilichopo kwa bahati mbaya. Kila kitu kina nafasi yake, kazi yake, na umuhimu wake katika mfumo wa maisha.

Hii ikanifanya nigeukie kwa mtu - kiumbe pekee anayeweza kufikiri, kutafakari, na kujiuliza maswali ya undani.

Niliamua kuchunguza kwa undani mitazamo ya dini kuhusu Mungu na kusudi la mwanadamu. Lakini kadri nilivyozidi kuchimba, ndivyo nilivyozidi kuchanganyikiwa. 

Niliona namna ambavyo dhana ya Mungu imefungwa ndani ya tafsiri finyu. Kila dini ina jina lake kwa Mungu: mara Yehova, mara Allah, mara Mola, mara Yesu, mara Roho. 

Kila kundi linaeleza kwa namna yake, likimfananisha Mungu na mtu - kana kwamba ni kiumbe mwenye sura, hisia, na mwelekeo wa kibinadamu.

Nilijiuliza: KAMA MUNGU NI WA WOTE, KWA NINI AWE NA MAJINA TOFAUTI KULINGANA NA IMANI? Je, Mungu ana dini? Kama hana, mbona wanaomfuata wamemgawa katika madhehebu na mafundisho yanayotofautiana sana? 

Na kama kweli Mungu ndiye chanzo cha maisha, basi mwanzo wa mtu ni upi? Je, kweli mtu wa kwanza alikuwa Adamu? 

Kwa nini baadhi ya mafundisho yakanieleza kuwa Adamu si mtu wa kwanza? Rejea Mwanzo 4:16. Na kama si yeye, ni nani? Alipewa utaratibu gani wa kuishi? Na nani alimfundisha?

Maswali haya yalinielekeza kwenye ukweli huu: siwezi kulielewa kusudi la mwanadamu kwa kupita tu katika mitazamo ya kidini, kwa sababu dini ni juhudi ya mwanadamu kumtafuta Mungu. 

Lakini Mungu kama ndiye chanzo cha uhai wote - yupo zaidi ya dini. Hana mipaka, hana itikadi, hana jina linaloweza kumtaja kikamilifu. 

Yeye ni Uwepo usio wa kawaida ambao hauwezi ukatathiminika na vinavyoishi. Chanzo kisichoelezeka kwa maneno ya kawaida.

Kwa hiyo, ili mtu atambue kusudi lake la kweli, ni lazima amjue kwanza Mungu mwenye vyote Kwanza! 

 Asitegemee majibu ya kurithi au ya kuaminishwa. Bali ajifunze kusikiliza ndani yake - kwa sababu ukweli wa kusudi lako hauko nje, uko nd
ani yako.

 Weka Oda Yako Sasa

Ikiwa umesoma makala hii na ndani yako kuna kiu ya kujua zaidi, ikiwa unataka kuendelea na safari ya kugundua na kuishi kusudi lako la kweli,

Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili yako!
Weka oda yako sasa na uanze safari ya kugundua maana ya uwepo wako kwa kina zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...