MATOKEO HAYAJI KWA TAMA - HUJA KWA MFUMO

Katika maisha, matokeo mazuri hayaji kwa sababu umetamani. Hapana.

Yanakuja kwa sababu umefanya kazi inayoleta matokeo hayo.

Huu ndiyo ukweli ambao watu wengi hawapendi kuusikia.

Kwa sababu mambo hayatokei kwa kutaka yatokee - hutokea kwa sababu umeandaa mfumo wa kuyafanya yatokee.

Kusema unataka kuwa tajiri ni sawa, lakini mchakato wa kujiandaa kuwa tajiri ndiyo huamua kama hilo tamanio linakuwa uhalisia.

Kusema unataka ndoa nzuri ni vizuri, lakini kuijenga hiyo ndoa ndiyo muhimu zaidi.

Kusema unataka maisha mazuri ni jambo la heri, lakini mchakato wa kuandaa maisha mazuri ndiyo unaamua kama utayapata au la.

Hii ndiyo hoja ninayotaka ikae moyoni mwako vizuri: Hakuna jambo linalotokea kwenye maisha kwa sababu umetaka litokee. Kila jambo linatokea kwa sababu umeandaa mfumo wa kulifanya litokee.

Watu waliofanikiwa duniani hawakufanikiwa kwa sababu walitamani mafanikio.

Wamefanikiwa kwa sababu walijiandaa - kisaikolojia, kiakili na kiroho.

Sasa angalia maisha yako: Je, matamanio yako yamewahi kugeuka uhalisia, au zimebaki kuwa ndoto zinazokupeleka kulala tu?

Na je, Unadhani utaendelea kuota mpaka lini?

Unadhani maisha yako yatabadilika kwa sababu tu unatamani yabadilike

Haijawahi kutokea, na haitaanza leo.

Kila mtu ana uwezo wa kufanya mambo yatokee -lakini si kila mtu anatumia uwezo huo.

Wengi wanasubiri mambo yatokee. Wengine wanayafanya yatokee.

Wewe uko upande gani?
Unataka mambo yawe sawa au unaweka mambo yawe sawa?

Tunachoishi nacho ni ulimwengu wa kanuni.
Na moja ya kanuni kubwa ni hii:

Kanuni ya Vichocheo na Matokeo

Kila kitu hutokea kutokana na sababu.
Hakuna matokeo bila kichocheo.
Hakuna mafanikio bila sababu.
Hakuna ndoa imara bila sababu.
Hakuna maisha mazuri bila sababu.

Nyuma ya kila matokeo, kuna vichocheo vinavyozalisha matokeo hayo.

Ukivijua na kuvifanyia kazi, unapata unachotaka.
Ukivipuuzia, unabaki na ndoto.

Hakuna siri nyingine.
Hakuna uchawi.
Hakuna ndumba.

Chochote unachotaka - tengeneza mfumo unaokipeleka kutokea.
Amini mfumo.
Dumu ndani yake hadi matokeo yajionyeshe.

Sijasema haya kwa sababu mimi ni mkamilifu.
Nasema haya kwa sababu hii kanuni imenijenga -kila hatua.

Safari yangu ya uandishi ilianza kwa kutumia kanuni hii.

Safari ya King Mentorship Program ni matokeo ya kufuata mfumo huu.

Ukiona kila siku napost maudhui, usifikiri napoteza muda au nakuchosha. Hapana.

Huo ndiyo mfumo wangu wa kujenga chapa, kukuza jina, kupata wateja na kuunganishwa na watu sahihi.

Tamaa bila hatua ni hadithi.
Tamaa bila mfumo ni muziki usio na ala.

Usiishie kutamani - tenda.
Wewe ni kifaa halisi cha kuzalisha maisha yako.

Ndimi, Mbulwa King’ung’e
Mawasiliano: 0744 284 329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...