ONYO! USIJARIBU KUBADILI HALI YAKO YA KIFEDHA KABLA HUJASOMA HII...
Habari rafiki,
Ni matumaini yangu uko salama na unaendelea vyema katika safari yako ya mafanikio!
Mimi ni mzima, mwenye nguvu na ari ya kukuongoza katika safari ya kuelewa elimu ya fedha kwa mtazamo wa kitaalamu na kiutu.
Leo, tuangalie sifa bainifu za fedha ambazo kila mtu anayetamani mafanikio ya kifedha lazima azielewe.
1. Fedha Inaongozwa na Kutengenezwa kwa Kanuni
Kila eneo la maisha ya MTU linatawaliwa na kanuni.
Na kama zilivyo sheria za asili, kanuni za fedha hazidanganyi.
Ukizitumia vizuri, zinakuletea matokeo chanya; ukizivunja, zinakukosesha utulivu wa kifedha.
Ukweli ni kwamba, kuna zaidi ya kanuni 20 za fedha, na mafanikio yako kifedha yatategemea namna unavyozitumia.
Tuchambue baadhi ya hizo muhimu:
1. Kanuni ya Kujilipa Kwanza
Kanuni hii inasema: Kwa kila pato unalolitengeneza, hakikisha unajilipa kwanza SEHEMU ya kumi ya pato Hilo kabla ya kufanya malipo mengine yote.”
Haijalishi una bili, kodi, au madeni - kipaumbele chako cha kwanza kinatakiwa kuwa wewe mwenyewe.
Kwa nini?
Kwa sababu umeajiri nafsi yako.
Unapofanya kazi, hufanyi kwa ajili ya kampuni au taasisi pekee, bali kwa ajili ya mustakabali wako.
Watu wengi hushindwa kufanikiwa kifedha kwa sababu hujilipa mwishoni au hawajilipi kabisa.
Na matokeo yake ni kukosa chochote cha kuwekeza au kutunza.
Kumbuka: mshahara wako si mafanikio; ni mbegu ya mafanikio.
Tenga angalau sehemu ya kumi ya pato lako, iweke kama malipo yako binafsi, kisha uwekeze sehemu hiyo kwenye mradi unaouelewa vizuri.
Uwekezaji huu utazaa faida (watoto wa fedha zako), kisha faida hizo zitazaa faida nyingine (wajukuu wa fedha zako).
Huo ndiyo mnyororo wa utajiri - unaoanza kwa kujilipa kwanza.
2. Kanuni ya Utunzaji na Ukusanyaji
Kanuni hii inafundisha kwamba:
“Siyo kipato unachoingiza ndicho kinachoamua mafanikio yako, bali kiwango unachoweza kutunza.”
Watu wengi hujificha nyuma ya hoja ya kipato kidogo, kumbe changamoto yao si kipato, ni nidhamu ya kifedha.
Anza kutunza angalau asilimia 10 hadi 20 ya kipato chako kila mwezi.
Kwa muda, utashangaa umejenga akiba yenye uwezo wa kuwekeza na kuzalisha fedha nyingine.
3. Kanuni ya Parkinson
Kanuni hii inaeleza: “Daimaatumizi huwa yanapanda ili kufikia kipato chako.”
Kwa lugha rahisi - kadri kipato kinavyoongezeka, watu wengi huongeza matumizi badala ya akiba.
Kanuni hii inakushauri *lkubaki na nidhamu ileile ya matumizi, hata kipato kinapoongezeka.
Ukijifunza kudhibiti matumizi, utaona mafanikio makubwa kifedha bila kujali kiwango cha kipato chako.
4. Kanuni ya Mlimbikizo
Kanuni hii inasema: “Utajiri mkubwa ni matokeo ya mlimbikizo wa fedha ndogo ndogo zilizokusanywa kwa mwendelezo ndani ya kipindi Fulani cha muda.”
Hii ndiyo siri ya watu wakubwa wa fedha duniani.
Siyo lazima uanze na milioni - anza na elfu moja tu kwa siku.
Ukifanya hivyo kila siku kwa mwaka mmoja, utakuwa na 365,000/= Na hiyo inaweza kuwa mbegu ya uwekezaji wako wa kwanza.
Kumbuka msemo huu wa hekima: “Haba na haba hujaza kibaba.” Hakuna kitu kidogo unapokifanya kwa mwendelezo.
5. Kanuni ya Mabadilishano
Fedha ni chombo cha mabadilishano.
Watu hulipa kwa vitu wanavyovithamini.
Kwa hiyo, ili kutengeneza fedha nyingi, tofautisha thamani yako.
Fanya kitu ambacho watu wanakihitaji lakini si rahisi kila mtu kukifanya.
Au kama wengine wanakifanya, kifanya kwa ubora wa aina Yake.
Thamani yako ndiyo kipimo cha kipato chako.
2. Fedha Ina Urahisi wa Kuitengeneza, Lakini Ugumu wa Kuidhibiti
Hapa ndipo wengi huangukia.
Watu wengi hutengeneza fedha kila siku, lakini wachache hudhibiti fedha zao.
Changamoto kubwa si kutengeneza, bali ni kuidhibiti fedha isiyopotee.
Wengi si maskini kwa sababu hawatengenezi, bali kwa sababu hawajui mbinu za kudhibiti matumizi.
Matumizi yasiyo na mpangilio, ununuzi wa hisia, na kutokuwa na bajeti ni sumu ya mafanikio ya kifedha.
Ili uwe huru kifedha, lazima ujifunze *uongozi wa fedha zako.
Kama hutaziongoza, zitakukimbia.
*Hitimisho*
Fedha ni mtumishi, si bwana.
Ukishindwa kuzidhibiti, zitakutawala.
Lakini ukielewa kanuni zake, zitakutumikia kwa uaminifu hadi kizazi chako.
Kumbuka: Mafanikio ya kifedha ni matokeo ya nidhamu, maarifa, na mwendelezo.
Anza leo, hatua moja kwa wakati, na uone nguvu ya mabadiliko ikianza ndani yako.
Ahsante sana kwa kuwa mwanafamilia wa masomo haya ya kifedha!
Ndimi Emmanuel Samuel King’ung’e
Mwl, Mwandishi, Muelimishaji katika Maendeleo Binafsi, Life Coach & Consultant
Founder - King Mentorship Program
📞 Wasiliana nami:
WhatsApp: +255 744 284 329 / +255 773 284 329
Comments
Post a Comment