Uishi Baada ya Kifo na Mwendelezo wa Maono ya Mtu Mfu
Wapo watu wanaoamini kwamba maisha huishia hapa duniani tu, na hakuna maisha baada ya kifo.
Ndio maana wakatunga msemo maarufu, “maisha yenyewe ndiyo haya haya.” YAANI unazaliwa, unaishi halafu unakufa na huo ndiyo mwisho wako.
Lakini ukweli ni kwamba kiumbe mtu alipewa elimu kuhusu alikotoka, namna ya kuishi akiwa hai, na hatima ya maisha baada ya kifo.
Ukiona unaishi bila kujua ulitoka wapi, jinsi unavyopaswa kuishi kimwili, na namna utakavyoishi kiroho baada ya kufa, basi pole sana.
Hapa huhitaji imani tu, bali uelewa wa kimungu juu ya kile alichofanya kwa viumbe vyake.
Leo hii, ukimuuliza mtu kuhusu maisha baada ya kifo, wengi watasema hayapo.
Wengine watasisitiza kwa ukakamavu: “Hakuna aliyekufa akarudi akatupa ushahidi.”
Wanajifanya makame kujua, kumbe hawajui hata kwa nini maisha yapo, wala kwa nini Mungu alifanya maisha Kwa vinavyoishi.
Wasijue, kumbe Mungu alitoa elimu kwa viumbe vyake. Kwa mfano kwa sisi viumbe Watu, elimu hiyo ilitolewa kwa MTU wa kwanza, ambaye alifundishwa kuhusu maisha baada ya kifo.
MTU huyo alifundishwa na muujiza wa Mungu uliofanyà uumbaji na ndiyo ulioandaa makao ya kiumbe kabla hakijaumbwa, na makao yake baada ya kufa.
Ndiyo maana kifo si mwisho, bali ni njia ya mpito kuelekea maisha mapya ya kiroho.
Ninaamini kuwa maisha hayaendi kumalizika kaburini, kwa sababu ndani yangu nina elimu na ufahamu wa kiroho unaonionesha kuwa naweza kuendeleza maono yangu hata baada ya kufa.
Kifo si adui; ni mlango wa kuingia kwenye hatua ya juu zaidi ya uhai.
Naelewa kuwa ninaishi kimwili kwa jukumu, kwa sababu mimi ni sayari ya viumbe wengine, niliyebeba viumbe vidogo vidogo ndani yangu, mbali na majukumu mengine ya kimaisha kama vile kuandika, kufundisha, kula, na kutenda mambo mengine ya lazima.
Lengo la Mungu kufanya maisha ni kwamba kiumbe afe katika uzee wake baada ya kukamilisha jukumu lake la KUISHI. Ndiyo maana mtu wa kwanza alipewa elimu ya kutunza nafsi yake.
Tatizo ni kwamba wengi hawana elimu ya kutunza nafsi zao - na mbaya zaidi, kila nafsi ina elimu yake binafsi.
Sasa fikiria hivi: ikitokea uhai wa mtu ukakatishwa ghafla kabla ya siku yake ya kufa, roho yake huondoka na kumbukumbu zote.
Kazi ya roho ni kuhifadhi kumbukumbu za maisha - ni kama kadi ya memori ya ndani inayorekodi kila tukio la maisha yako.
Kwa hiyo, kama mtu alikuwa na maono ya kuleta haki, amani au usawa katika taifa lake, halafu akafa kabla hajayatimiza, roho yake huendeleza maono hayo kiroho kupitia watu waliopo hai.
Kwa nini aendeleze vision yake?
Kwa sababu roho hupata faraja kwa kuona yale aliyoyaanza alipokuwa kimwili yakitimia.
Ni kama vile unavyohisi furaha unapokamilisha jambo ulilopanga. Kumbuka, roho hutoka na tabia za mtu - kwa hiyo hufanya haya yote ili ipate faraja ya kuona maono yakitimia.
Ndiyo maana tunasema mtu fulani ana “spirit ya kupambana” - mara nyingi ni kwa sababu anaguswa na nguvu za kiroho zinazotaka kuona maono fulani yakitimia.
Watu kama hao ni vyombo vya roho na huwa wanasaidiwa kiroho katika safari yao.
Mimi si mwanasiasa, lakini chukukulia mfano tundu lisu, alipigwa risasi 16 akapona kurudi kaendelea na harakati, kawekwa NDANI lakini Bado yuko ngangari kitu ambacho siyo kawaida kwa MTU kama wewe.
Unanafikiri anafanya vile bila sababu kuna vision za watu wengine kuhusu Tanzania zinakamilishwa kupitia yeye.
Sasa tufanye watu wamefia nchi kwa vision ya kudai haki, wamekufa vision haijatimia, nini kinafuata ninyi mliopo hai kimwili mtakuwa vyombo vyao vya wao kukamilisha vision.
Wale wenzetu wa dini utasikia wao ni vyombo TU, kwa hiyo hata ninyi mtatumika Kama vyombo vya kutimiza maono ya Roho hizo.
Sasa hapa Ndiyo wenzetu wakampachika mungu kuwa ni Roho wasijue kwamba Roho zilifanywa na Mungu mwenyewe na yeye hatuumii roho kwa sababu si kiumbe na haishi na si hai wala si MFU..
Hili litufundishe kuua siyo kutatua tatizo ni kutengeneza TATIZO mtakaloshindwa kudhibiti kwa sababu hakuna aliye kimwili atakayepambana na roho na kuishinda.
Kwa hiyo unaweza ukashangaa unazima moto kwa kutumia petroli.
Kwa hiyo kuna maisha baada ya kifo, ndiyo MAANA kuna wengine huwa mnasemeshwa na roho za vizazi vyenu.
Hiyo iwape picha kuwa kuna maisha baada ya maisha ya kimwili na ufufuo upo..
Wenu kijana mdogo.
Mbulwa King'ung'e
Comments
Post a Comment