Ukiachwa Achika: Siri Kali ya Kuacha Kung’ang’ania Mtu Asiyekutaka...
“Yaani mimi maisha yangu bila Fulani haiwezekani… Yeye ndiye alikuwa kila kitu kwangu.”
Hayo ni maneno yanayotoka kwa watu ambao mapenzi yamewachanganya kiasi cha kusahau kwamba hata kabla ya mahusiano hayo, maisha yao yaliendelea vizuri tu.
Kwa sababu , kabla ya huyo mtu kuingia kwenye maisha yako, uliishi, ulipumua, ulifanya kazi, ulijipanga - na uliendelea tu bila kupasuka.
Lakini leo hii, mtu akikuacha unasingizia dunia yote imekugeuka.
Unajifanya huna uhai.
Unajifanya huna thamani.
Unajifanya huwezi tena.
Tatizo ni kwamba wengi wamejigeuza kuwa vipenzi ving’ang’anizi.
Hawataki kuachika, hawataki kukubali, na mbaya zaidi – mahusiano wanayong’ang’ania hayana mizizi.
Waliingia kwa kukurupuka kama vitenzi vikurupushi, halafu mwisho wa siku mwenzako kageuka na kuwa kitenzi kikwamizi, wakati wewe umebaki kuwa kitenzi king’ang’anizi.
Matokeo? Unageuka kipenzi king’ang’anizi.
Wewe kubembeleza; mwenzako anakukomesha.
Wewe kutuma SMS; yeye kuzifuta bila kuzisoma.
Wewe kupiga; yeye “anakata” simu kwa makusudi.
Siku nzima inbox - matone ya machozi badala ya maneno.
Mahusiano ambayo hayakuwa na msingi hata kidogo, leo unayabeba kichwani kana kwamba ni kampuni uliyoisajili TRA.
Kaka/dada yangu, mbona unajipeleka motoni?
Wenzako wanakimbia moto wewe unaukumbilia?
Unazima moto kwa petroli kweli?
Kama mtu amekuambia hakutaki - mshukuru.
Ndiyo, mshukuru!
Kuna watu wanaishi kwenye mahusiano ya kinafiki miaka mitano wakidanganywa “I love you” wakati vitendo vinaandika “I don’t want you” kwenye mioyo yao.
Wewe angalau umeambiwa ukweli.
Huo ni ukombozi, sio kipigo cha moyo.
Swali ni: Kama mtu hakutaki, kwanini kung’ang’ania? Ukiona mtu hakutaki, jua kuna kitu hakifai kwake.
Jifunze kusikiliza, kirekebishe, uboreshe nafsi yako - lakini sio kwa ajili yake, bali kwa ajili ya mtu sahihi atakayekuja.
Usijidanganye kuwa mtu anabadilika kwa sababu ya mapenzi. HAPANA.
Watu hubadilika kwa sababu ya maamuzi yao wenyewe, sio kwa sababu umelia sana, umeumia sana au umeandika paragraph 17 za kuomba msamaha.
Ndugu yangu, ukiachwa - ACHIKA.
Ukikataliwa - SIMAMA.
Ukidharuliwa - ONDOKA.
Ukiteswa - JIKOMBOE.
Hukubaliki kwake? Haimaanishi hutakubalika kwa mwingine.
Hebu fikiria: Ni mara ngapi tumesikia mtu kafukuzwa kazi eti “hafai,” halafu baada ya wiki chache tu akapata kazi yenye mshahara mkubwa, adabu kubwa, na mazingira bora kuliko kule alikokataliwa?
Huo ni ushahidi kuwa: Tunapoteza vitu vizuri ili tupate vitu vilivyo bora zaidi.
Lakini ili upate bora zaidi, lazima ukubali kupoteza.
Sasa wewe unamng’ang’ania mtu ambaye:
— Anakuumiza badala ya kukufariji
— Anakudhalilisha badala ya kukuthamini
— Anakurudisha nyuma badala ya kukusukuma mbele
— Anakutesa badala ya kukuponya
Kama amekufanyia hayo, basi si wako, na wala haumfai.
Anachostahili si kung’ang’aniwa - anastahili kupuuzwa, kama anavyokupuuza mwenyewe.
Hii ndiyo ile tunasema: Yeye akimwaga ugali, wewe mwaga mboga. Hakuna kucheka na maumivu yako.
Naandika haya si kama mtu aliyeamka leo na kusema “ngoja niandike.” La hasha!
Naandika kama mtu aliyepitia, aliyeshuhudia, aliyefanya utafiti, na anayeona namna watu wanavyogeuka wafungwa wa mapenzi yasiyowapenda.
Ukweli ni huu: Watu wengi sana wako kwenye mahusiano, lakini hawapendwi.
Wanateseka kimyakimya.
Wanaishi kama wafungwa wanaosukuma siku, sio wapenzi wanaoishi furaha.
Cha kushangaza? Watesaji wao ndio wanaowang’ang’ania zaidi.
Upate kufahamu hili: kila eneo la maisha lina misingi yake. Ukiikosa misingi ya mahusiano, lazima mambo yabomoke, yajichanganye, na mwisho wa siku uishi kwenye maumivu ambayo yalipaswa kuepukika.
Ndiyo maana ninahitaji watu wawili tu - wale ambao wako tayari kujifunza, kupokea, na kuifanyia kazi misingi sahihi ili wapendwe kwa uzito, adabu na thamani.
Wadada watapewa kipaumbele, kwa sababu ndio wamekuwa wakiumia zaidi, kung’ang’ania wanaowatesa, na kuamini kwamba wanaweza kuokoa mahusiano ambayo tayari yamevunjika kabla hayajaimarika.
Kama upo tayari kupokea ushauri wa msingi, utakaokujenga na kukurejesha kwenye uhalisia wako, basi fanya jambo moja tu:
Tuma neno MSINGI kwenda namba 0744284329.
Ukiachwa achika.
Ukikataliwa shukuru.
Ukiumizwa jifunze.
Ukidharauliwa ondoka kwa miguu yote miwili.
Hiyo ndiyo safari ya kuelekea kwa mtu anayekupenda bila kukupunguza.
Ndimi Mbulwa King'ung'e
Comments
Post a Comment