USIMTENDEE MWENZAKO YALE USIYOTAKA KUTENDWA KANUNI YA DHAHABU YA MAISHA

“Dunia haitaharibiwa na watu waovu, bali na wale wanaotazama uovu huo bila kusema wala kuchukua hatua.”  Albert Einstein

Je, umewahi kujiuliza kwa nini dunia ya leo imejaa maumivu, migogoro isiyoisha, chuki za ndani zisizotamkika, na watu waliokata tamaa?

Jibu lake ni moja tu: Tumeacha kuwa watu kwa ajili ya watu wenzetu.

Tumejivua utu. Tumevua huruma. Tumevaa vinyago vya unafiki na ubinafsi. 

Tumesahau kwamba kila anayepumua ni kioo kinachotuonyesha sisi wenyewe - na tunayomtendea ni kama tunajitendea wenyewe.

Chanzo Kikuu cha Maumivu ya Watu Wengi

Leo hii watu hawalalamiki kwa sababu ya ukosefu wa pesa pekee. Watu wanalalamika kwa sababu ya kutendwa visivyo.

Wanaume wanasaliti wake zao na wanacheka, lakini wakisalitiwa wanataka dunia isimame.

Wanawake wanadanganya hisia na kuchuna wanaume, lakini wakifanyiwa hivyo wanavunjika mioyo.

Rafiki, kwanini utende kitu ambacho huwezi kustahimili wewe mwenyewe ukifanyiwa?

Kama huwezi kukubali kuumizwa, kwa nini unaumiza? Kama huwezi kukubali kudanganywa, kwa nini unadanganya?

Huo si ujanja. Huo ni unafiki.

Uhusiano Umevunjika Kwa Sababu Tunakomoana

Leo hii ndoa nyingi zimevunjika. Si kwa sababu watu hawawezi kupendana, bali kwa sababu wamejifunza kukomoana kuliko kusameheana.

Mahusiano yamegeuka uwanja wa kisasi. Hakuna tena upendo wa kweli. Kila mtu anaficha ajenda. Hili linazaa kizazi kipya cha watu wenye hofu, chuki, na huzuni zisizoponyeka.

Matokeo yake?

Wanaume wanachukia wanawake.
Wanawake wanawadharau wanaume.
Jamii inajenga ukuta badala ya daraja.

Ukweli Huu Unauma Lakini Unaponyesha

Watu wengi wanatembea na majeraha ya kiakili kwa sababu ya kutendwa visivyo na wale waliowaamini.

Wanaume wanaumia kimyakimya. Wanawake wanalia gizani. Wazazi hawazungumzi na watoto wao. Majirani hawasalimiani. Ndugu wamegeuka maadui.

Lakini je, hii ni lazima iwe hivi?

Hapana.
Inawezekana kabisa kurekebisha. Tuanze kwa kanuni moja:
Usimtendee mtu mwingine kile ambacho wewe mwenyewe huhitaji kutendewa.

Nguvu ya Mawazo na Athari za Kisaikolojia

Unapomfikiria mtu kwa chuki, kisasi, au maumivu, akili yako ya ndani (subconscious mind) haijui kama unamfikiria mtu mwingine. Inaamini unajifikiria wewe.

Ndiyo maana unajikuta ukiwa na msongo wa mawazo, huKinyongo huua m hasira zisizo na sababu, na hata maradhi ya ajabu ajabu.

Kinyongo huua mwili kabla hakijaua roho.
Msamaha si zawadi kwa mwingine. Ni tiba ya nafsi yako.

Utu Unapotangulia - Maisha Yanaweka Mizizi ya Amani

Mtu anayejua kustahimili anapenda amani kuliko ushindi. Mtu anayejua kuwapenda wengine haishi kwa kujilinganisha.

Tungekuwa na dunia tofauti leo kama kila mtu angejitahidi kuwa chanzo cha furaha kwa mwingine.

Jiulize: Kama kila mtu angekuwa kama mimi, je, dunia hii ingekuwaje?

Tuanze na Wewe: Punguza Hasira. Punguza Wivu. Samehe. Acha Kinyongo.

Tenda wema bila kutegemea shukrani. Mpende mtu bila kuogopa kutopendwa. Sema neno jema bila kutegemea kurudishiwa.

Unapowatakia wengine mema - furaha, afya njema, mafanikio - unavivutia hivyo hivyo kwenye maisha yako.

Fikra zako ni mbegu. Na kila mbegu huzaa matunda ya aina yake.

Tunaweza Kujenga Dunia Bora… Tukianzia na Moyo Wako

Usisubiri viongozi wabadilike. Usisubiri dini ifundishe zaidi. Usisubiri sheria ziandikwe upya.

Anza wewe - kwa kufuata kanuni ya dhahabu:
"Tenda yale ambayo nawe ungependa kutendewa."

Wasifu wa Mwandishi:

Emmanuel Samuel King’ung’e
Ni Mwalimu wa Maisha (Life Coach), Mwandishi, na Mwasisi wa King Mentorship Program. 

Ana uzoefu mkubwa katika kuhamasisha watu kujitambua, kuondoa vizuizi vya ndani, na kuishi maisha yaliyojaa kusudi, maadili, na mafanikio ya kweli. 

Kupitia programu yake, amewasaidia vijana, watu wazima, na viongozi kupata mwelekeo mpya wa maisha.

Jiunge na King Mentorship Program Leo!

Ikiwa umeguswa na makala hii - basi fahamu kuwa huo ni mwanzo tu. King Mentorship Program ni jukwaa la mafunzo ya kina yatakayokusaidia:

✅ Kujitambua na kuvunja vizuizi vya ndani
✅ Kujenga maadili na maamuzi yenye tija
✅ Kujifunza usimamizi bora wa fedha
✅ Kutengeneza mfumo wa maisha unaoleta furaha na uhuru wa kweli
✅ Kuishi kwa kusudi na ushawishi

Jiunge nasi leo kwa kutuma ujumbe WhatsApp kupitia namba:
📲 0744284329 au 0773284329

Kumbuka:
Dunia inahitaji watu wanaojali. Ulimwengu unahitaji sauti yako. Mtu anahitaji mtu mwingine - si adui, bali rafiki. Anza leo kwa kutenda mema.

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...