Uwezo Wa Ndani Unaotengeneza Matokeo Ya Nje

Leo kijana wenu niko hapa na jambo zito, jambo linalohitaji utulivu wa kiwango cha juu.

Kwa hiyo, tafadhali… vuta kiti, kaa kwa kutulia, halafu pumua polepole.

Na kama una popcorn, endelea tu kutafuna; unaweza hata kushushia soda baridi bila haraka.

Nataka tuzungumze kama marafiki wawili waliokutana kwenye chemchemi ya ukweli.

Kwa sababu jambo la leo linaingia moja kwa moja kwenye kiini cha mafanikio ya ya kiumbe MTU, kile ambacho wengi wanakitamani, lakini wachache wanakitafakari kwa undani.

Wacha nikuulize swali moja rahisi lakini zito:
Kwa nini kila mtu anatamani mafanikio, lakini si kila mtu anayafikia?

Ndiyo msingi wa mazungumzo yetu ya leo.

Kila mtu anatamani kufika hatua fulani maishani. Kila mtu anatamani siku moja historia yake itajwe mahali kwa adabu kubwa. 

Hii si hulka ya watu pekee, hata viumbe vingine vimeumbwa na hamu ya kupanda juu.

Lakini leo nataka kuzungumza na wewe, mtu ambaye ndani yaki kuna kiu ya kupata matokeo makubwa kuliko unayoishi sasa.

Kitu cha kwanza unachopaswa kujua ni kwamba, Matokeo hayaji kwa sababu umetamani, umeomba, au umeota. Matokeo huja tu pale ambapo umejijengea uwezo wa kuyazalisha.

Matokeo mazuri ni zawadi unayoipata kutokana na aina ya mtu unayekuwa ndani ya nafsi yako.

Kwa lugha nyepesi tuseme Kuna matokeo ambayo hayatakaa yatokee kwenye maisha yako kama utaamua kubaki yule yule kila siku.

Na ndiyo maana unahitaji kuwa MTU mwenye uwezo wa kubadilika ili kuendana na dunia inayokua kwa kasi…

Kwa sababu ulimwengu wa leo hautaki tu watu wanaotamani, bali watu wanao jitengeneza kulingana na viwango vipya.

Kile ulicho nacho jana hakiwezi kukusukuma kwenye matokeo unayotaka leo.

Unapobadilika, unaongeza uwezo; unapoongeza uwezo, unaongeza uwezekano; unapoongeza uwezekano, ndipo matokeo mapya huzaliwa.

Kwa MAANA hiyo, Maisha hayakulipi kwa sababu ya kile unachotamani, bali kwa sababu ya mtu unayekubali KUWA.

Dunia imebadilika sana. Mafanikio ya leo yanahitaji mtu anayeweza kubadilika, si mtu anayeshikilia tabia za jana, fikra za jana na uwezo wa jana.

Matokeo mapya hutengenezwa na mtu mpya.

Kila hatua mpya unayotamani, kila kiwango kipya unachotamani kufikia, kinahitaji kwanza kubadilika kwa ndani.

Ukibaki na utambulisho ule ule, utapokea maisha yale yale.

Lakini unapokubali kubadilika, ndipo uwezo wa kuzalisha matokeo mapya unafunguka.

Huu ndiyo msingi wa kila mafanikio makubwa duniani.

Moja ya kanuni kubwa ya watu wakubwa duniani ni hii: wanalinganisha kile wanachotaka na uwezo wao wa kukizalisha.

Badala ya kulilia matokeo fulani, jiulize kwa uaminifu wa kiroho na kiakili:

Je, nina uwezo wa kuyatoa matokeo haya?
Ninajiweza?
Ninajimudu?
Nimeiva kiasi cha kubeba majibu ninayotamani?

Kabla hujasema “nataka kutengeneza milioni moja kwa mwezi,” jiulize: Je, nina uwezo wa kuzalisha milioni moja kwa mwezi, au ninakana ukweli kwa ndoto za mchana?

Hakuna “bahati mbaya” kwenye ulimwengu huu.
Tunaishi kwenye mfumo wa vichocheo na matokeo ya moja kwa moja.

Kuna biashara zinadidimia.
Kuna taasisi hazikui.
Kuna familia hazipigi hatua.
Kuna watu wanapambana kila siku lakini maisha yameganda kama maji kwenye barafu.

Si kwa sababu hawataki.
Si kwa sababu hawana bidii.
Ni kwa sababu hawajui namna ya kuzalisha matokeo wanayoyataka.

Kufanikiwa kifedha ni zao la thamani unayoibeba ndani yako.

Ukiwaona watu hawako tayari kukulipa, tambua kuwa bado hujajenga thamani inayolipika.
Mtu yule yule hawezi kuingia daraja tofauti la mafanikio.

Kujenga familia iliyo thabiti kunahitaji misingi.
Usipoyajua misingi ya mahusiano na ndoa, amani itakuwa ndoto ya mbali.

Kufanikiwa kimaisha kunahitaji pia msingi wa kiroho. Bila kusimama katikati ya ukweli wa kiroho, unaweza kujikuta unavurugikiwa hata unapopambana na uwezo wa juu.

Ndio maana wengine huanza kupata mwanga, ghafla mambo yanarudi nyuma. Si kwamba hawana kazi, nguvu au akili. La hasha!

Wanapungukiwa upande wa kiroho, na mifumo ya ndani inakuwa dhaifu kupokea vichocheo vya mafanikio.

Kwa hiyo, ili uwe mtu wa matokeo makubwa, hakikisha unajijengea sifa hizi:

1. Ujitambue - Jua wewe ni nani na kwa nini upo duniani.
2. Jiimarishe kiroho - Mjue Mungu wa kweli, si viabudiwa vya tamaduni za watu.
3. Jifunze misingi ya uchumi na fedha - Thamani inazalisha fedha, si maombi pekee.
4. Jenga uhusiano mzuri na watu - Fedha imo mifukoni mwa watu, si mawinguni.
5. Kuwa na mentor au life coach - Mtu wa kukusimamia, kukukosoa, kukusogesha mbele.
6. Usiache kujiboresha - Kila siku jikweze, jikuze, jiongeze.

Kwa msaada zaidi, wasiliana nami,
au jiunge na King Mentorship Program - mahali ambapo unatengenezwa kuwa mtu mwenye uwezo, uthubutu na nuru ya kufanya mambo yatokee, si kwa bahati, bali kwa uwezo halisi wa ndani.

📞 Mawasiliano: 0744 284 329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...