FEDHA SIYO OMBI — NI HESABU, NI MAAMUZI, NI AKILI...
Kuna jambo moja watu wengi hawajafundishwa kuhusu fedha: fedha ni mfumo wa mabadilishano.
Na mfumo huu haukui kwa maombi—unakua kwa maarifa, uelewa wa namba, na uamuzi sahihi wa kiakili.
Fedha haina uhusiano wa moja kwa moja na Mungu. Wala Mungu hagawi fedha.
Ndiyo maana hata yule MTU wa Kwanza mnayemjua, hakuwahi kupewa fedha na Mungu.
Kwa sababu fedha si riziki ya kiungu—ni zao la mahusiano kati ya viumbe.
Kuimiliki fedha hakuhitaji kufunga, kujinyima, au kujitesa.
Kwa sababu mgawao wa fedha hauko kwa Mungu—uko mikononi mwa watu wenzako.
Na hebu nikukumbushe jambo moja: Fedha inachapishwa Uswisi.
Na Mungu hayupo Uswisi. Yeye yupo huko aliko—na huko aliko hakuna makao.
Makao aliyafanya kwa ajili yetu sisi tunaoishi kimwili na kiroho.
Hivyo basi, kama fedha ni mgawao kutoka kwa kiumbe kimoja kwenda kwa kingine, basi sheria ni moja tu:
👉 lazima uwape watu thamani fulani, ndipo wao wakupe riziki yako.
Kuwa na fedha si suala la kuomba kila siku.
Ni suala la: kuelewa namba, kuelewa nyakati ulizomo, na kujua namna ya kuizungusha fedha ili ijizalishe.
Sasa acha nikuulize swali la kiutu uzima, si la mtu wa maombi: "Nikikupa milioni moja leo, nikupe miaka mingapi ili iwe milioni kumi?'
Hili swali halihitaji uanze kusema:
“Roho wa Bwana niongezee…” Hapana.
Linahitaji akili iliyofundishwa kucheza na namba.
Unatakiwa ujue: ni fursa gani utawekeza, fedha utazungushaje, na mtaji wako utafanya kazi vipi.
Si kufanya vitu kwa kubahatisha huku ukisema:
“Mungu atatenda.”
Hapana. Mungu ana utenzi—huo ndiyo muujiza wake. Yeye hatendi. Ninyi viumbe vyake *ndiyo mnatenda.
Mmepewa: uwezo, nguvu, maisha, dunia na vyote vilivyomo.
Bado mnataka Mungu atende badala yenu?
Hebu kuweni hata na aibu.
Akili kubwa, ikipewa milioni moja, inajua itazalisha kiasi gani cha fedha.
Baada ya kujua hicho kiasi, ndipo inafanya hesabu.
Mfano wa wazi kabisa:
Tuseme milioni moja inakutengenezea 100,000/= kwa mwezi.
10,000,000 ÷ 100,000 = miezi 100
Mwaka una miezi 12:
Chukua: miezi 100 ÷ 12 = miaka 8.3
Maana yake:
👉 miaka 8 na miezi kama 3–4 kutengeneza milioni kumi.
Umeona? Sijaomba. Sijafunga. Sijaita mbinguni.
Nimefanya hesabu.
Hapo ndipo unatambua: nina uwezo gani wa kuzalisha kila mwezi na nitachukua muda gani kufika ninapotaka.
Ndiyo maana ninasema kwa msisitizo:
ifundishe akili yako kucheza na namba.
Zijue namba. Na ujue namba hizo zinamaanisha nini.
Kufanikiwa si bahati.
Ni uelewa wa namba + maamuzi sahihi + uthubutu wa kuchukua hatua.
Hakuhitaji kuomba riziki.
Kunahitaji: ujue ni watu wangapi watakupa riziki, baada ya kuwapa thamani gani, na riziki hiyo iwe gawo lako.
Naitwa Mbulwa King'ung'e.
Ninaendesha King Mentorship Program — programu za utambuzi binafsi.
Ninatoa pia elimu ya fedha ambayo hukufundishwa shuleni.
Sihubiri. Sikupi matumaini hewa.
Nakufundisha akili ifanye kazi.
Nahitajika na watu watano tu — si wengi.
Watu watano tu watakaonipa riziki
kwa kubadilishana na thamani halisi nitakayowapa.
Usiwaze mara mbili.
Matajiri hufikiri haraka na huamua mapema.
Njoo inbox.
Nipe riziki 😅 nile ninenepe, maisha yaendelee,
na wewe uanze safari ya kupata riziki kwa kuwapa wengine thamani.
📞 Mawasiliano: 0744 284 329
Comments
Post a Comment