KWA NINI MALENGO YA WATU WENGI HAYAFANIKIWI?
Ukweli ambao wengi hawako tayari kuusikia. Kila mwaka jambo lile lile hurudiwa.
Watu huandika malengo mapya. Hujiapia mabadiliko mapya. Hujiambia, “mwaka huu nitabadilika.”
Lakini mwaka unaisha—maisha yale yale,hali ile ile, visingizio vile vile.
Iwapo kweli malengo yangetimia kama yanavyoandikwa, dunia hii leo ingekuwa tofauti kabisa.
Tungeona watu wengi wakitoka chini kwenda juu, familia zikikaa sawa, na jamii zikijengwa na watu waliojitambua. Lakini hilo halitokei.
Na bila shaka, na wewe mwaka huu umejiwekea MALENGO—ya kifedha, mahusiano, afya, elimu au biashara.
Lakini licha ya nia njema, wengi hushindwa kuyatekeleza.
Na sababu si ukosefu wa ndoto. Sababu ni ukosefu wa uelewa wa kina wa maisha na mfumo wake.
Kama umeweka malengo, soma sababu hizi kwa umakini. Usipofanya marekebisho, utajikuta ukishindwa tena—sio kwa bahati mbaya, bali kwa sababu hauzingatii mfumo.
Malengo hayashindikani kwa sababu ni makubwa.
Yanashindikana kwa sababu wewe hubaki mdogo kuliko yanachohitaji.
Ukipanda mbegu ya ndizi, usitarajie kuvuna embe.
Zifuatazo ni sababu kubwa zinazopelekea malengo mengi kutotekelezwa:
1. Unabaki kuwa mtu yuleyule
Kama umefika hapo ulipo kwa sababu ya yule uliyekuwa, usitarajie kufika mbali zaidi bila kubadilika.
Ukibaki mtu yuleyule wa jana, utapata matokeo yale yale ya jana.
Usiandike malengo makubwa bila kubadili utambulisho wako.
Usiishie kuazimia malengo makubwa—kuwa aina ya MTU anayehitajika ili kuyatimiza.
Malengo hutimizwa na aina fulani ya watu—sio kwa bahati, bali kwa tabia.
2. Orodha kubwa ya malengo yasiyo halisi
Mtu mmoja unataka afanye kila kitu! Ajabu iliyoje.
Unataka pesa, ndoa, afya, biashara, elimu—vyote kwa mwaka mmoja.
Hayo si MALENGO, ni mkanganyiko.
Lenga kidogo, fanya kwa ukubwa.
Ni bora lengo moja kubwa likatekelezwa vizuri kuliko malengo kumi yasiyokwenda popote.
Malengo mengi yasiyo halisi ni mzigo na chanzo cha msongo wa mawazo.
Rafiki, lengo moja kubwa linaweza kubadilisha maisha yako yote.
3. Kukosa mbinu na mikakati madhubuti
Hakuna lengo linalojitekeleza lenyewe.
Ukisema “nitajenga nyumba”—hilo ni lengo.
Lakini nyumba haijijengi.
Malengo bila mikakati ni maombi yasiyo na mwelekeo.
Weka mikakati, ratiba, na hatua za kila siku zitakazokupeleka huko.
4. Kukosa uthabiti wa maamuzi
Haya ni maisha yako.
Bado unamsubiri mwajiri, baba, mama au mwenzi akuamlie?
Wewe upo kwa ajili ya nafsi yako—na wao wapo kwa ajili ya nafsi zao.
Rafiki, hakuna anayejenga maisha yako kwa niaba yako.
Kesho yako inahitaji uamuzi wako, si ruhusa ya mtu.
5. Kukosa sanaa ya mwendelezo
Moto wa Januari unawaka sana. Februari umeisha.
Hujui? Matokeo makubwa yanapatikana kwa mambo madogo yanayofanywa kwa mwendelezo.
Maisha hubadilishwa na mambo madogo yanayorudiwa kwa nidhamu
Bila sanaa ya mwendelezo, malengo yako yatabaki kuwa ndoto.
6. Dharura za muda mfupi
Kusimamishwa kazi kunatokea. Kuugua kunatokea. Kuachwa kunatokea.
Tatizo si tukio—tatizo ni akili isiyoandaliwa kuyapokea.
Haya yote huathiri malengo na mustakabali wako.
Ndiyo maana nasisitiza elimu ya saikolojia—ili uweze kuhimili misukosuko bila kuvunjika.
Bila uelewa huu, changamoto ndogo zinakuwa sababu ya kukata tamaa kubwa.
7. Visingizio visivyo na msingi
Unapanga vizuri: Tarehe 25 Januari nitaweka akiba.
Siku inafika. Limbic system inakupeleka kwenye starehe—pombe, wanawake, nguo, miruko.
Unajisemea: “Maisha ni mafupi.”
Ndiyo, ni mafupi—lakini kisingizio hakitekelezi lengo.
Lengo lako litabaki pale pale, na baadaye litahitaji muda na nguvu kubwa zaidi.
8. Upotevu wa muda.
Mitandao ya kijamii na burudani zisizo na tija zinaua ndoto kimya kimya.
Saa 3 TikTok. Saa 2 Instagram. Saa 1 porojo.
Halafu unasema huna muda wa kujijenga?
Kuangalia mapaja nje nje kunaweza kuburudisha—lakini ni hatari kwa malengo yako.
Freeze TikTok.
Freeze Facebook.
Fungua mara moja kwa wiki kama huna agenda ya maana.
9. Kukata tamaa mapema
Ukisikiliza motivational speakers, utafikiri mafanikio ni kulala na kuamka.
Ukiingia kwenye utekelezaji, mwezi mmoja tu umechoka.
Mafanikio si miujiza—ni mchakato unaoumiza kabla haujapendeza.
Calm down. Relax.
Usiwe na papara—la sivyo utawachukia mentors na waelimishaji bure.
10. Kuishi kwa hofu na hali ya unyonge
Unajiona hutoshei.
Unajiona si bora.
Hiyo ni sauti ya mazingira, sio ukweli.
Unaweza. Unastahili kuishi maisha yaliyojaa furaha, amani na mafanikio.
Pambana kuyatengeneza—maisha hayajitengenezi yenyewe.
11. Sababu za kiroho
Hapa wengi hawapendi kusikia.
Unaabudu kiumbe mwenzako, umekiita Mungu.
Roho za watenda mabaya, wachawi, waganga—vyote unavihusisha na kushindwa kwako.
Fikiria: Mungu gani aliletwa na wakoloni, na bado unaona madhara ya ukoloni?
Kwa nini jina Mungu lilikuwepo Afrika kabla yao, lakini wao wakaleta mfumo mpya wa kuabudu viumbe?
Usipomjua Mungu wa KWELI, na bado unashikilia hofu ya malaika na majini, bado uko ndani ya mfumo wa kiroho unaokudhoofisha.
HITIMISHO
Malengo hayatekelezwi kwa: kuandika, kuomba, au kusikiliza motivational clips.
Yanatekelezwa kwa: mabadiliko ya akili,mifumo sahihi, na mwongozo mkali unaokukataa kujidanganya.
Kama umechoka kuzunguka duara,
kama unataka mtu akuambie ukweli bila kukupapasa,
📩 Njoo inbox.
Tutafanya one-on-one coaching.
Usije na stori.
Usije na lawama.
Njoo na hela yako TU.
Wako,
Mbulwa King’ung’e Founder wa King Mentorship Program.
📞 0744284329
Comments
Post a Comment