MGOGORO WA UTAMBULISHO, IMANI PANDIKIZI, NA UPOTOSHAJI WA DHANA YA MUNGU...
Leo ndugu wanauana bila hata kujua walikotoka.
Ona wanavyojichanganya, wamesahau kabisa asili yao.
Wanabeba mavazi, fikra, na mitazamo isiyo ya kwao—kama fahari.
Wamesahau walikotoka...
Wamefundishwa kudharau vya kwao.
Wanabeba fikra, mavazi, na mifumo ya imani isiyo yao, kisha wanaivisha jina la “ukweli wa milele”.
Wametolewa kwenye misingi ya utu wa asili yao, wakaingizwa kwenye mifumo iliyobadilisha mabaya yaonekane mazuri, na mema yaonekane ya kishenzi.
Hawajui asili yao. Wamegeuzwa watumwa wa mila na tamaduni za wengine.
Hawajui hata maana ya majina yao ya ukoo.
Hawajui maana ya majina ya makabila yao.
Hawajui kwanini waliitwa hivyo.
Kwao, hayo yote ni upumbavu—hasa yakilinganishwa na imani pandikizi zinazowaharibu kiakili kila siku.
Wamegawanyika makundi kwa makundi.
Kila kundi linajiona ndilo sahihi. Kila kundi linahukumu lingine. Kila kundi linadai linafunguo za mbinguni—na kuliona lingine litaishia motoni.
Ukiwauliza: Moto uko wapi?
Hawana majibu.
Ukiwauliza: Lengo la Mungu ni nini kama mwisho wake ni kuwachoma viumbe aliowaumba?
Hawana majibu.
Ukiwauliza: Kama alitaka tuokolewe, kwanini alimruhusu shetani aje atudanganye ili atupeleke motoni?
Hawana majibu.
Ukiwauliza: Kama nimekoseshwa na kiumbe aliyeruhusiwa kunidanganya, kunichoma moto si kunionea?
Hawana majibu.
Hizo ndizo simulizi za Mungu aliyeletwa na watu wa Ulaya kupitia misheni za ukoloni.
Kwa ukatili walioufanyiwa babu zanguu, huwezi kunishawishi tena kuhusu huyo Mungu waliomleta wale watu.
Nilikubali kudanganyika kwa muda. Lakini sasa akili yangu imepevuka. Nilikuwa nautafuta ukweli—na sasa nimeupata.
Mungu si jambo dogo kama anavyochorwa.
Amegeuzwa kituko, kwa sababu kila upumbavu unaofanywa na viumbe wajinga na wafubafu kiakili unapachikwa kwake.
Wanampa taswira finyu: eti anabebwa kwenye machela na malaika.
😅
Lakini ukiangalia uzito wa dunia moja tu, ukaacha mabilioni ya sayari nyingine—je, kweli kuna viumbe vinavyoweza kumbeba muumbaji wa vyote?
Jamani, Mungu si jambo dogo.
Wengine wamempa mpaka watoto.
Wanasema ana Mtoto, tena alipatikana kwa kuingilia mahusiano ya watu kwa kutuma Roho.
Lakini kama vitu vyote vimekuwepo kwa sababu yake, na yeye ndiye muumbaji wa kila kitu, angejipaje kazi hiyo ilhali ana uwezo wa kufanya chochote bila taratibu hizo?
Leo kila mtu anasema lake.
Wengine wako tayari hata kuua ili “kumtetea Mungu.”
Mungu huyo ni dhaifu kiasi gani hadi ahitaji watetezi wa damu na visu?
Siku utakapoelewa Mungu ni nini, na mola ni nini, ndipo utaelewa kwanini huwa nasema: Si kila kinachoabudiwa na halaiki ni Mungu.
Mamola ni viongozi wakubwa wa malaika na majini.
Hawa ndio wanaobebwa kwenye machela.
Hawa ndio walitaka kuabudiwa.
Hawa ndio waliotuma malaika kuwaletea ujumbe wa kuwaabudu wao—yaani muabudu mamola wao.
Hapo ndipo utumwa ulipoanza, kisha ukageuzwa kwa hila na kuitwa “utumwa wa Mungu.”
Kwa hiyo ukisikia mtu anasema katumwa na Mungu, elewa huyu ni muongo.
Mungu hana watumwa.
Mamola ndio wana watumwa.
Kumbuka: Mungu si mshirika.
Mamola wako wengi—ndiyo maana hoja zao zinakinzana.
Ukielewa tofauti ya Mungu na mola, utaelewa kwanini duniani kuna vurugu nyingi, na kwanini hakuna anayeweza kudadavua mambo kwa kina.
Watu wa Ulaya walidanganywa na viumbe hawa wa majini na malaika.
Wakageuzwa watumwa kwa muda mrefu.
Baadaye wakagundua kuwa hao viumbe walikuwa wabaya na wezi. Wakaanza kujitoa kwenye mikataba yao.
Lakini kabla hawajaondoka kabisa, wakaleta taswira za mamola wao Afrika kupitia dini.
Na ndicho kinachoendelea hadi leo.
Usishangae kiongozi akisema:
“Ili umuamini Mungu, lazima uwe chizi.”
Ni kweli kabisa—kwa sababu ukitumia akili, utaona hakuna cha maana.
Mungu gani anayehitaji kwanza uwe chizi ili umuamini?
Kwanini basi asingewaumba machizi tu wote hapa duniani?
Kama ulikuwa hujui, malaika na majini ni viumbe kama ninyi.
Wana majukumu ya kusimamia sayari zao, kama ninyi mlivyo hapa duniani.
Wanazaa. Wanafanya ngono. Wanakufa na kuzikwa kama ninyi.
Na wakizubaa, hata vibao unaweza kuwanasa tu.
Hawa ndio waliokuja kuvuruga utu wa watu wa duniani kupitia mawakala waliowapata miongoni mwa watu wa Ulaya.
Nikisema namjua Mungu, elewa.
Kama una hoja kubwa zaidi ya hii—njoo inbox.
Ukiumia, umia. Lakini huo ndio ukweli.
Baki na hasira.
Baki na ujinga.
Nimemaliza kusema.
Ndimi Mbulwa King'ung'e
Mawasiliano: 0744 284 329
Comments
Post a Comment