“Si Kila Mtu Ni Wako: Siri ya Kuishi, Kujenga, na Kuepuka Kukata Tamaa...”
Kuna watu—lakini si kila mtu ni wako.
Ukisikia mtu akisema “kuna watu na kuna viatu”, mara nyingi huwa ameshindwa kutofautisha hoja. Maisha hayagawanyiki kwa dharau, bali kwa uelewa.
Ukweli ni huu:
Si watu wote wataunga mkono unachofanya.
Si watu wote watakuwa wafuasi wako.
Si watu wote watanunua bidhaa au huduma yako.
Si watu wote watajitolea kwa ajili yako.
Hilo ni jambo la kawaida kabisa.
Mtu kutokuunga mkono hakumaanishi yeye ni kiatu—la hasha.
Huenda hakuhitaji. Au huenda anahitaji, lakini hajui kuwa wewe ndiye jibu lake.
Kukupuuza kwake hakupunguzi thamani yako.
Ni lazima ukubali jambo moja muhimu:
Kuna watu hawatakuelewa, hata kama utakuwa mzuri kiasi gani.
Hata kama utakuwa bora kiasi gani.
Hata kama utajitahidi kiasi gani.
Hata kama utakuwa mwema kiasi gani—bado hawatakuelewa.
Na hilo si kosa lako.
Watu hao si wako. Moyo wao, imani yao, na utegemezi wao umeelekezwa kwa mtu mwingine, si kwako.
Na asije mtu akakutisha kwa usemi usemao:
“Usimtegemee mtu.”
Anayesema hivyo hajui kanuni za kuishi.
Jiulize kwa uaminifu:
Kama usingewategemea wazazi wako, ungekuwa wapi?
Kama usingetegemea mwalimu au mentor aliyekujenga, ungekuwa wapi?
Kama usingetegemea kazi inayokupa mshahara, ungekuwa wapi?
Niambie, kuna kiumbe gani kisichotegemea Mungu? Kipo wapi? Nionyeshe.
Ndugu msomaji, mfumo wa maisha umejengwa juu ya kutegemeana.
Biashara yako ipo kwa sababu watu wanaitegemea.
Huduma yako ipo kwa sababu watu wanaitegemea—na wewe unawategemea wao.
Basi hoja ya “tusitegemee watu” ipo wapi?
Ndani ya kutegemeana huko, kuna hekima moja ya msingi sana: Ni lazima ujue ni watu gani waliokusudiwa waje wategemee kile ulichojaaliwa.
Uelewa huu utakusaidia: Kuepuka kukata tamaa. Kuacha kulaumu watu. Kuacha kuomba kuthaminiwa na wasiokusudiwa.
Badala yake, jitengeneze msimamo.
Vuta watu wanaofanana na wewe.
Katika maisha haya nimejifunza kuchagua watu.
Watu wanaoelewa ninachofanya.
Watu wasiopenda kudanganywa.
Watu wanaotumia akili.
Watu wasiotaka ushabiki, bali wanataka kuelewa.
Watu wanaotafuta ukweli wa kuishi—ulio juu ya cheo, kazi, mshahara, au fedha.
Hao ndiyo watu ninaowatafuta.
Sitaki watu wanaopenda kudanganywa.
Mwezi huu wa kwanza, nilipunguza watu wengi sana.
Si kwa sababu walikuwa wabaya—la hasha.
Bali kwa sababu hawakuwa wanaunga mkono ninachofanya.
Nilipunguza ili kila mmoja aende mahali anapolingana.
Ndipo nikaanza upya.
Leo ninajenga jamii inayojitambua.
Jamii inayoweza kujiongoza, kujisimamia, na kujitawala.
Haya yote yanatekelezwa kupitia: KING MENTORSHIP PROGRAM.
Karibu uwe sehemu ya familia hii.
Hapa, ukweli wa kuishi kiutu ndiyo kipaumbele chetu cha kwanza.
Ndimi Mbulwa King’ung’e
Founder – King Mentorship Program
📞 Mawasiliano: 0744 284 329
Comments
Post a Comment