“Ukomo wa Maisha Yako Upo Kwenye Kiwango Chako cha Uelewa...”


Watu wengi hudhani kwamba maisha yanapimwa kwa umri, bahati au mazingira tuliyotokea. 

Lakini ukweli ambao mara nyingi hauzungumzwi ni huu: maisha hupimwa kwa kiwango cha uelewa wa mtu.

Hakuna anayepiga hatua kubwa kimaisha bila kwanza kupanua uelewa wake, na hakuna anayekwama bila sababu, huwa amekwama mahali uelewa wake ulipokomea.

Ndiyo maana utaona watu wanafanya kazi kwa bidii ile ile, wanatumia muda ule ule, lakini matokeo yao yanatofautiana sana. 

Tofauti hiyo haipo kwenye nguvu ya mwili wala bahati, ipo kwenye kile wanachokijua, wanachoelewa, na wanachokifanya na uelewa huo. 

Makala hii si ya kukutia moyo kwa maneno matamu, bali ni ya kukufanya ujitazame kwa kina, uhoji kiwango chako cha uelewa, na utambue kwa nini maisha yako yako pale yalipo—na nini hasa kinakuzuia kwenda mbali zaidi.

Ukweli ni huu: hakuna mtu anayeenda mbali zaidi ya kiwango chake cha uelewa kilipokomea.

Kwa maana hiyo, ukomo wa maisha yako upo kwenye kiwango chako cha uelewa.

Hii ina maana rahisi sana: ukijua vitu vichache utapiga hatua ndogo, ukijua vitu vingi utapiga hatua kubwa.

Na ndiyo maana tofauti kati ya tajiri na maskini haipo kwenye kutengeneza fedha. Wote hutengeneza fedha. Tofauti ipo kwenye uelewa.

Mmoja anaelewa namna ya kudhibiti fedha, mwingine haelewi. Na hapo ndipo tunapotofautiana kimaisha.

Ndugu yangu, fahamu hili: sote tunazaliwa sawa.

Tunazaliwa tukiwa uchi, tunazaliwa tukiwa wajinga, na tunazaliwa tukiwa na hofu.

Hakuna anayezaliwa akiwa na fedha mkononi, hakuna anayezaliwa akiwa na nyumba mbili, hakuna anayezaliwa akiwa na magari wala mali.

Tunakuja sawa.

Tofauti huanza pale maisha yanapokupa nafasi ya kujifunza, halafu wewe ukaamua utatumia au hutatumia ulichojifunza.

Nawajua watu waliotoka kwenye mazingira magumu zaidi yako, lakini leo wamepiga hatua kubwa kimaisha.

Walifanya nini tofauti? Hawakuelewa jambo moja.

Mara baada ya kuzaliwa na kupata kibali cha kuendelea kuishi hapa duniani, tunapitia aina mbalimbali za elimu.

Elimu ya dini. Elimu ya kitaaluma. Elimu ya biashara. Elimu ya dunia.

Haijalishi utaanza na ipi.
Kinachopima maisha yako si elimu uliyonayo, bali ulichofanya na elimu hiyo.

Kwa sababu maana ya elimu ipo kwenye matokeo, na matokeo hutokana na vitendo.

Ndiyo maana ilisemwa: “maarifa ni nguvu” lakini ukweli ni huu: maarifa yaliyotumika ndiyo yenye nguvu.

Watu wengi wamesoma, lakini hawana ujuzi.

Kwa nini? Kwa sababu hawajawahi kuyaweka maarifa yao kwenye vitendo.

Na hapa ndipo watu wengi huchanganyikiwa.

Kwa sababu: maarifa ni kujua, lakini ujuzi ni kufanya.

Na ni kwa kufanya ndipo: unaboreka, unajijenga,
na unapokuwa bora.

Unapofanya kitu mara kwa mara, watu wanaanza kukuona.

Wanakujua.

Na wanapokujua, unaanza kuishi kwenye akili zao.

Hapo ndipo sifa zako zinajengwa.

Na pale unapotatua changamoto za watu kupitia ujuzi wako, unaanza kuzama mfukoni mwao.

Si kwa nguvu, bali kwa thamani.

Fedha humfuata yule anayepunguza adha za watu.

Na watu wakishapendezwa na kile unachofanya, wanakuunganisha na wengine.

Hapo ndipo mtandao wako unajengwa.

Kumbuka hili: mtandao wako wa watu ndiyo kipimo cha thamani yako.

Cha kushangaza ni kwamba, watu wengi wanalalamika maisha ni magumu, ilhali wanajua vitu vingi, lakini hawajaamua kuvifanya.

Tambua hili pia: kuna kusoma ili uajiriwe, na kuna biashara ya utaalamu wako.

Mwalimu anaweza kubobea kwenye eneo fulani na kulipwa nje ya mshahara.

Daktari anaweza kutumia ujuzi wake kusaidia watu zaidi ya hospitali.

Msingi ni mmoja tu: jifunze, tumia, fahamika, lipwa, na panua mtandao.

Ndugu yangu, kabla hujanisoma zaidi, jiulize haya maswali matano:

1. Unajua nini mpaka hapo ulipofikia?
2. Unaweza kufanya nini kutokana na unachokijua?
3. Ni nani wanaokujua?
4. Una nini?
5. Dunia inakutambuaje?

Ninakupa jibu langu kama ushuhuda.

Nimejifunza. Nikaweka kwenye vitendo. Nikapata ujuzi. Nikafahamika. Nikalipwa. Nikapanua mtandao.

Ndiyo maana leo: naandika, nashauri, nasimamia watu, naelimisha, na nawekeza.

Nimeandika vitabu vitano.

Nimeanzisha King Mentorship Program.

Nimegusa maisha ya watu wengi.

Sio kwa sababu nilikuwa bora Unataka kujua nilianzaje?

Majibu yapo hapo juu.

Unataka kujua ulipo ulipo, uende wapi?

📩 Karibu inbox ukiwa umejipanga tayari.

Hakuna huduma ya bure.

Mbulwa King'ung'e
Founder – King Mentorship Program.

Mawasiliano: 0744284329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...