“Ulibomolewa Kiakili, Sasa Ni Wakati wa Kujengwa Upya...”
Kuna dhana moja muhimu sana katika maisha ya watu inayoitwa blank slate, au kwa lugha ya kifalsafa tabula rasa.
Kwa mara ya kwanza nilisikia neno hili nikiwa shule ya msingi. Lakini matumizi yake yalikuwa mabaya na ya kuumiza.
Mwanafunzi akifanya kosa, aliitwa “tabula rasa”—kwa maana ya mtu asiye na akili, asiyejua chochote, asiye na thamani. Tafsiri hii ilikuwa ya kupotosha na ya kuumiza.
Matokeo yake yalikuwa makubwa kuliko tulivyodhani.
Watoto walijiona hawafai. Walijiona wajinga. Walijiona hawana uwezo. Wengine walilia, wengine walinyamaza, lakini wengi wao waliendelea kuishi na imani hiyo hadi utu uzima.
Hadi leo, bado kuna watu hawaamini katika mawazo yao, si kwa sababu hawana akili—bali kwa sababu waliambiwa hawana.
Cha kushangaza ni hiki:
👉 hata huyo mwalimu aliyekuwa akitamka maneno hayo alizaliwa akiwa tabula rasa pia.
Tofauti ni moja tu—yeye aliingiziwa taarifa.
Akaingiza maarifa ya ualimu, akaingiza lugha, fikra, kumbukumbu na uzoefu. Kama asingepata taarifa hizo, angebaki kuwa tabula rasa maisha yake yote.
Hapa ndipo ukweli ulipo:
👉 Tabula rasa si tusi. Ni hali ya mwanzo.
Nilielewa maana halisi ya dhana hii mwaka 2021, baada ya kusoma kitabu Change Your Thinking, Change Your Life cha Brian Tracy.
Ndani ya kitabu hicho ndipo nilipokutana kwa kina na nadharia ya tabula rasa, iliyoasisiwa na mwanafalsafa David Hume.
Kwa mujibu wake: “Hakuna mtoto anayezaliwa akiwa na ufahamu au uelewa wa jambo lolote.”
Hii ina maana kwamba: Kila mtoto huzaliwa akiwa hana kumbukumbu. Hana tafsiri. Hana imani. Hana hofu. Hana mipaka ya fikra.
👉 Kila kitu huingizwa baada ya kuzaliwa.
Kila tendo analofanyiwa mtoto huingia kama taarifa. Kila neno analoambiwa hurekodiwa kama ukweli.
Ndiyo maana: akiambiwa “huwezi” — anajifunza kushindwa. Akiambiwa “hustahili” — anajifunza kujidharau. Akiambiwa “huna akili” — anaishi kulingana na hilo.
Hasa maneno haya yanapotoka kwa watu anaowaamini—wazazi, walimu, viongozi wa dini na jamii.
Kwa maana hiyo basi, kupitia maneno na matendo, tunawatengeneza watoto wetu.
Na huo utengenezaji unaweza kuwa wa: kuwajenga au kuwaharibu.
Taarifa za awali ndizo huamua mtu atakuwa nani baadaye.
Kuna watu wanaojiamini, wanaothubutu, wanaobuni—kwa sababu waliingiziwa taarifa sahihi mapema.
Na kuna wengi, hasa Afrika, wanaoamini hawawezi, hawastahili na hawana uwezo—si kwa sababu ni kweli, bali kwa sababu hawakuingiziwa taarifa sahihi.
Walizaliwa na uwezo huo, lakini: walikaripiwa, walifokewa, walidhibitiwa na walikatishwa tamaa.
Na kwa bahati mbaya, mfumo wa elimu umechangia kwa kiwango kikubwa.
Walimu wengi waliopaswa kuwa nguzo ya kumjenga mtoto kisaikolojia, kwa kusomea saikolojia, waliishia kuisoma ili kufaulu mitihani na kupata ajira, badala ya kuielewa kwa kina kwa lengo la kujenga akili ya MTU.
Matokeo yake, saikolojia ikawa cheti cha kazi, si chombo cha ukombozi wa fikra.
Hapo ndipo unamsikia akisema kwa ujasiri usio na aibu: “Uelewe usielewe, mshahara utaingia.”
Na dhamira yake hujitakasa kwa sentensi moja: "Nikuhangaikie sana, kwani wewe ni mwanangu?”
Lakini matokeo yake ni taifa lenye watu waliovunjika kiakili.
Usije ukaona jamii imeharibika hivi ukadhani ni bahati mbaya. Watu waliandaliwa kuwa hivi—kupitia: elimu, malezi, jamii na dini za mapokeo.
Ndani ya dini, wengi wamefundishwa: wasitumie akili, wasubiri wakati wa bwana ufike, waamini kwamba “Bwana atatenda. N.k”
Kumbe Mungu alimpa kiumbe uwezo atende. Kwa MAANA yeye Mungu huwa hatendi bali ana utenzi ambao ndiyo muujiza wake.
Mungu hayupo kwenye nyakati— yeye ndiye aliyefanya wakati kwa ajili ya viumbe vyake.
Na MTU huyo aliyeharibiwa hivi anaweza kuwa ni huyu anayesoma ujumbe huu.
Huyu ndiye ambaye jamii na taifa linamtegemea.
Sipo hapa kukuhukumu.
Lakini jiulize kwa uaminifu: Umechangia nini duniani? Na mchango wako umetokana na fikra huru au fikra zilizoharibiwa? Unatumia uwezo wako kamili au umewekewa mipaka ya fikra?
Kwa mfumo huu tulionao, tunategemea wapi kupata: wabunifu? wagunduzi? viongozi jasiri?
Ndiyo maana ninapozungumza kuhusu King Mentorship Program, sizungumzii jambo dogo.
Haikuanza kwa kukurupuka.
Ilianzishwa kama jibu la tatizo la fikra zilizoharibiwa.
Ni zaidi ya elimu ya darasani. Ni program ya kujenga upya akili ya MTU: ajitambue, ajiamini, atumie uwezo wake na achukue nafasi yake katika jamii.
Ni ujenzi wa: jamii bora, taifa bora na dunia bora.
Kama umefika mwisho wa ujumbe huu na kuna kitu ndani yako kimegusa, ujue huu si msisimko—ni mwito wa mabadiliko.
👉Karibu uwe sehemu ya kizazi kinachojielewa kwa kujiunga na kozi za King Mentorship Program.
Ndimi Mbulwa King’ung’e
Founder – King Mentorship Program
📞 0744 284 329
Comments
Post a Comment