Dunia ya Mafumbo: Jela Isiyoonekana ya Fikra za Watu...
Kuna kitu kinaitwa fumbo.
Kuishi katika ulimwengu uliojaa mafumbo yanayofumba akili ya mtu isifanye kazi inavyotakiwa ni mateso makubwa sana.
Mateso haya si ya mwili tu, bali ni ya fikra, utambulisho, na maana ya kuishi.
Mafumbo mengi yanayoenezwa duniani hayajatokana na Chanzo halisi cha uhai—yaani Mungu mwenye vyote.
Badala yake, ni matokeo ya maisha baada ya viumbe kupoteza ukweli.
Walipoupoteza ukweli, wakaunda bunifu zao wenyewe.
Na kwa kuwa bunifu hizo hazikuwa na ukweli, wakaamua kuwafumba watu ili wasielewe.
Fumbo likawa zana ya kuficha upungufu wa maarifa.
Ndiyo maana mtu anapouliza maswali ya msingi— Maisha ni nini? Yalianzaje? Sisi ni nani?—huambiwa: “Hilo ni fumbo.”
Huambiwa haliwezi kuelezwa kimwili, bali lina maana ya kiroho.
Lakini hapa ndipo mgogoro ulipo: mtu anaishi kimwili, anaugua kimwili, anakufa kimwili, anaishi katika jamii kimwili—lakini anaambiwa majibu yapo nje ya uhalisia anaouishi.
Ni sawa na kumwambia mtu aliye gizani: “Usiulize kuhusu mwanga, utauelewa baada ya kufa.”
Lakini ukweli ni huu: Siyo viumbe vyote vilipoteza ukweli.
Wapo waliouhifadhi.Wapo wanaojua ukweli kuhusu maisha: yalikotoka, yalivyosambaa, na sisi tulivyopatikana.
Kuishi ndani ya mafumbo kunamnyima mtu haki ya msingi ya kujua asili yake.
Na asipojua asili yake, hujishikamanisha na tamaduni za wengine, simulizi za wengine, na hofu za wengine.
Ndiyo maana wapo watu ambao hawajawahi kujiona kuwa wao ni watu kamili—si kwa sababu hawajaumbwa, bali kwa sababu wamefundishwa kujitazama kupitia mafumbo.
Wakati huohuo, tunadai Mungu hakujifumba.
Jaribu kufikiria hili kwa akili huru: Umezaliwa duniani. Hujui maisha ni nini. Hujui upo juu ya nini.
Hujui uhai unatoka wapi. Halafu aliyekuumba aanze kujificha kwako.
Hivi, utawezaje kujielewa kwa kweli?
Ndiyo maana leo: Watu wengi wanaishi bila kujua wao ni nani. Wanachofanya hakilingani na walivyo. Maamuzi yao yanapingana na asili yao.
Ni kwa sababu huwezi kujua ulipo kama hujui ulipotoka.
Tunaambiwa mafumbo yapo ili adui asijue siri.
Lakini swali la msingi ni hili: Kama Chanzo cha uhai ndicho chenye nguvu zote, adui ana nguvu gani ya kukifanya kijifiche?
Je, mwenye nguvu humficha mwenyewe?
Au anayejificha ni yule asiye na uhakika wa ukweli wake? Je, si ajabu?
Haya si maswali ya kufuru.
Ni maswali ya akili iliyokataa kulemazwa.
Kama hujui, ipo Elimu ya Kiutu.
Elimu hii:
Inazungumzia Chanzo cha Utu
Inaeleza msambao wa watu duniani
Inasisitiza umoja wa watu wote
Haina mafumbo—kwa sababu ukweli hauhitaji kufichwa.
Fumbo ni kwa mjinga. Mwerevu hulitambua, hulivua, na huliacha.
Baki kwenye mafumbo, utaendelea kubahatisha maisha.
Chagua ukweli, utaanza kujielewa.
Ukitaka kujielewa wewe ni nani, ulipotoka, na kwa nini upo— karibu kwenye Elimu ya Kiutu.
Ndimi Mbulwa King’ung’e
📞 Mawasiliano: 0744 284 329
Comments
Post a Comment