“IMANI: Programu Iliyokuendesha Kabla Hujajitambua...”


Kuna kitu kinaitwa imani.

Wengi hulifikiria ndani ya mifumo ya dini. Lakini ukweli ni huu: imani haikuanza na dini. Imani ni mfumo wa ndani wa kila kiumbe. Ni muundo wa kisaikolojia unaoundwa kabla hujapata umri wa kuchagua.

Imani ni matokeo ya kuishi.

Ni zao la mazingira. Ni tafsiri ulizojifunza kabla hujajua kuwa unajifunza. 

Ni programu iliyoandikwa ndani ya akili yako ya chini ya fahamu (subconscious) kupitia marudio ya maneno, matukio na hisia.

Ulikuwa mtoto. Hukuchambua. Hukupinga. Hukupima. Ulimeza.

Kila neno uliloambiwa. Kila hali ya kifedha uliyoiona. Kila hofu ya wazazi wako. Kila malalamiko ya nyumbani. 

Kila misemo kama; “hiyo si yetu”, “maisha ni magumu”, “sisi hatuwezi”, “tajiri lazima ana ujanja”.

Hayo yote hayakupita tu. Yalikujenga.

Taratibu ukaanza kuunda taswira ya maisha. Taswira ya wewe ni nani. Taswira ya kinachowezekana na kisichowezekana.

Hukuchagua kuamini. Uliundwa kuamini.

Kama wazazi wako ni Waislamu, uliingia Uislamu. Kama ni Wakristo, uliingia Ukristo. Ungezaliwa Antarctica, ungeamini mfumo mwingine kabisa.

Hii haimaanishi imani ni batili — inaonesha kwamba mazingira yana nguvu ya kuunda mfumo wako wa ndani.

Na si katika dini tu.

Hata kuhusu fedha. Hata kuhusu mafanikio. Hata kuhusu thamani yako binafsi. Hata kuhusu ukubwa wa ndoto zako.

Kila kitu kina mizizi kwenye mazingira yaliyokulea.

Saikolojia inaita hii conditioning. Uongozi wa fikra unaita hii identity formation.

Lakini kwa lugha rahisi — ulipewa hadithi kuhusu maisha, ukaikubali kama ukweli.

Kama ulikulia uhaba, ukaamini maisha ni mapambano.

Kama ulikulia kukatishwa tamaa, ukaamini ndoto ni za wachache.

Kama ulikosolewa kupita kiasi, ukaamini wewe si wa kutosha.

Na imani inapokaa muda mrefu, inageuka kuwa utambulisho.

Ndipo mtu anaanza kusema:“Mimi niko hivi.” “Mimi siwezi hivi.” “Mimi si wa mambo makubwa.”

Lakini ukweli ni huu — hiyo si wewe. Hiyo ni programu.

Na programu inaweza kubadilishwa.

Swali ni hili:

Kwa nini kwako imekuwa ngumu kuamini unaweza?

Kwa nini ndani yako kuna sauti inayokuambia hustahili?

Kwa nini unapokaribia mafanikio fulani unajikuta unajipuuzia mwenyewe?

Kwa sababu ndani yako kuna imani iliyojificha inayosema: “Hii si ya kwangu.”

Uliaminishwa utajiri ni dhambi. Uliaminishwa ukubwa ni kiburi. Uliaminishwa kuota ndoto kubwa ni kujiona.

Lakini jiulize — je, hayo ni kweli halisi au ni tafsiri ulizorithi?

Ukweli usiopingika ni huu: ulizaliwa ukiwa na uwezo. Ukiwa na akili yenye nguvu isiyo na mipaka. Ukiwa na ubunifu. Ukiwa na uwezo wa kujifunza, kubadilika, na kufanikiwa.

Hakuna mtoto anayezaliwa akijua hawezi.

Lakini kadri unavyokua, sauti za nje zinaanza kuwa kubwa kuliko sauti yako ya ndani. Watu wanakupima kwa vigezo vyao. Wanakupa mipaka yao. Wanakujengea hofu zao.

Na taratibu unakubali.

Ndipo maoni ya wengine yanapogeuka kuwa ukweli wako.

Ndipo mtu anaanza kutapatapa. Anahama kutoka kundi moja kwenda lingine. Anajaribu biashara moja, kisha nyingine. Anasoma hiki, kisha kile. Lakini ndani hakuna uthabiti. Hakuna imani thabiti ya “Ninaweza.”

Kumbuka kanuni hii: Unapokea kadri ya unavyoamini.

Kuamini ni kukubali jambo kuwa kweli hata kabla hujaliona kwa macho. Na akili inapokubali jambo kuwa kweli, inaanza kutengeneza ushahidi wa kulithibitisha.

Ndiyo maana mtu anayeamini maisha ni magumu hupata ushahidi wa ugumu kila mahali. Na anayeamini maisha yana uwezekano huanza kuona milango kila mahali.

Habari njema ni hii:

Kama imani zilijengwa, zinaweza kuvunjwa.
Kama programu iliandikwa, inaweza kufutwa na kuandikwa upya.

Kama uliaminishwa huwezi, unaweza kujifunza kuamini unaweza.

Tatizo si uwezo wako. Tatizo ni mfumo wa ndani unaoongoza maamuzi yako bila wewe kujua.

Na hapo ndipo mabadiliko halisi yanaanzia — si kwa kubadilisha mazingira kwanza, bali kwa kubadilisha namna akili yako inavyotafsiri mazingira.

Huo ndiyo msingi wa King Mentorship Program.

Hatuji kukuambia uamini nini.
Hatuji kubadili dini yako.
Hatuji kukupachika falsafa mpya kwa nguvu.

Tunakuja kukufundisha kuitumia akili yako.
Tunakuja kukuonesha jinsi ya kuitambua imani iliyojificha ndani yako.

Tunakuja kukusaidia kuvunja mipaka uliyopewa bila ruhusa yako.

Akili ikipevuka, utaanza kujiamini.
Ukijiamini, utaanza kuchukua hatua kwa uthabiti.

Ukichukua hatua kwa uthabiti, matokeo hayatakuwa bahati — yatakuwa sheria.

Hitaji kubwa la MTU si fedha kwanza.
Si mtaji. Si connection.

Ni kuamini katika uwezo wake mwenyewe.

Tunarejesha imani yako iliyopotea. Tunarejesha hadhi yako ya ndani. Tunakuunganisha tena na nguvu uliyozaliwa nayo.

Kwa sababu hujazaliwa kwa bahati mbaya.
Hujazaliwa kuishi maisha ya wastani kwa kulazimishwa.

Umezaliwa ukiwa na uwezo wa kufanya mambo yatokee.

Na wakati umefika wa kuandika programu mpya.

Mimi ni Mbulwa King'ung'e, mwanzilishi wa *King Mentorship Program.

Mawasiliano: 0744284329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...