“Je, Wewe Ni Kiongozi wa Ndani au Ni Kiongozi wa Nje? Hii Ndiyo Safari Yako ya Kweli...”
Kabla hujaendelea, lazima niwe muwazi kwako. King Mentorship Program si kwa kila mtu.
Si kwa mtu anayehitaji mafanikio ya haraka. Si kwa anayehitaji motivation ya muda mfupi. Si kwa anayehitaji mbinu za pesa haraka bila kujijenga ndani.
Kama unatafuta njia rahisi, majibu mepesi, au matokeo ya haraka bila kazi ya ndani — ni bora uishie hapa.
Lakini kama uko tayari kuanza na nafsi yako kabla ya kuanza na maisha yako, kama uko tayari kujihoji, kujikosoa na kubeba uwajibikaji wa maisha yako, basi endelea. Hapa ndipo safari yako inaanza.
Kuna kitu kinaitwa hali na mapito katika maisha.
Wengi wamefundishwa kuhusisha hali hizi moja kwa moja na Mungu, na kusahau kabisa jukumu lao la kuongoza maisha yao wenyewe.
Ukweli ni huu: kila mtu ni kiongozi, lakini si kila mtu ni kiongozi sahihi. Usahihi wa uongozi hautokani na cheo tu; unatokana na maarifa sahihi.
Kama huna maarifa sahihi kuhusu Mungu,
huna maarifa sahihi kuhusu maisha, huna maarifa sahihi kuhusu wewe mwenyewe na kusudi la kuumbwa kwako —basi wewe ni kiongozi ambaye utajipotosha kwa mikono yako mwenyewe.
Kiongozi asiyejijua ni rahisi kulaghaiwa na viongozi wengine waliopotea, akajikuta akitegemea habari zisizo za kweli, zisizomhusu.
Tatizo kubwa ni hili: hatufundishwi sisi ni nani. Tunatengenezwa tuwe watu fulani. Hatufundishwi tuangalie tuna nini ndani — tunapewa mafunzo ya nje.
Matokeo yake tunaishi watu wawili tu wanaokinzana. Mtu wa nje anapingana na mtu wa ndani.
Mtu wa ndani anajaribu kusema ukweli, lakini mtu wa nje anataka sifa, pesa au kukubalika. Na hapo ndipo msongo wa ndani unapoanza, kuchanganyikiwa, kuharibiwa na habari za wengine.
Hii si kwa sababu ya Mungu. Lahasha. Ni kwa sababu kiongozi wa maisha yako kapotoshwa, akajikuta akitegemea nje, akifurahia uso wa nje huku ndani akiteketea.
Amepewa kazi, lakini kanyimwa kusudi. Anafanya kazi kwa kulazimishwa. Anaumiza hata wengine kwa sababu ya kazi. Haya yote hayaji kwa bahati mbaya — ni kutokujua kwanini anaishi.
Moja ya swali unalotakiwa ujiulize ni hili, kati ya Mungu, shetani, na matashi yako — nani kweli anaharibu maisha yako?
Katika King Mentorship Program tunamtenganisha Mungu na mtu. Tunafundisha kwamba Mungu aliumba kiumbe akampa akili timamu.
Akili ipo, lakini si kila mtu anaitumia. Hapa tunafundisha kutumia akili timamu, kutumia maarifa, si kuishi kwa kuzingatia uso tu. Hivyo basi, hii si programu ya kila mtu.
Kama umeona umepotezwa na taarifa za dunia, kama hujawahi kujichuja, kama hujui tena unaongozaje maisha yako — basi unahitaji kuwa kiongozi wa ndani kwanza, kabla ya kuongoza nje.
Na kama umefika mpaka hapa, kuna mambo mawili yameanza kuwa wazi: King Mentorship Program si kwa kila mtu, na kama bado unasoma, kuna kitu ndani yako kimeamka.
Hii si safari ya majibu ya haraka. Ni safari ya kuuliza maswali ambayo hukuwahi kujiuliza. Si kwa ajili ya kukufariji — bali kukujenga. Si kwa ajili ya kukuchekesha — bali kukuweka sawa.
Kama uko tayari kujenga mizizi kabla ya matunda, kubeba wajibu wa maisha yako bila kulaumu mazingira, hatua inayofuata si kusoma makala nyingine.
Hatua inayofuata ni kuwasiliana na sisi. Si kwa kuuliza bei, si kwa kuomba maelezo marefu, bali kuthibitisha kuwa uko tayari kuanza safari ya ndani.
Mbulwa King’ung’e, Mwanzilishi — King Mentorship Program
📞 0744 284 329
Comments
Post a Comment