“Mafanikio Bila Utambuzi Binafsi Ni Adhabu..."
Kabla hujaendelea kusoma, ni muhimu niwe muwazi KWAKO.
King Mentorship Program si kwa mtu anayehitaji mafanikio ya haraka, si kwa mtu anayehitaji motivation ya muda mfupi, wala si kwa anayehitaji mbinu za haraka za kupata pesa bila kujijenga ndani.
Kama unatafuta njia rahisi, majibu mepesi au matokeo ya haraka bila kazi ya ndani,
ni bora uishie hapa.
Lakini kama uko tayari kuanza na kujijenga katika nafsi yako kwanza kabla hujajijenga kimaisha, kama uko tayari kujihoji, kujikosoa na kuchukua uwajibikaji wa maisha yako, basi endelea — hapa ndipo safari yako inaanza.
Kuna kitu kinaitwa mafanikio ya haraka. Wengine wanayaita get rich quick schemes. Mimi nayaita mtego wa kizazi.
Nimekutana na watu wengi sana wanaotaka kufanikiwa kwa haraka—ndani ya mwezi mmoja wapate matokeo ambayo watu wengine wameyapata baada ya miaka ishirini hadi arobaini ya kujijenga.
Tatizo siyo kutamani mafanikio. Tatizo ni kutotaka kujengwa ili kuyabeba.
Ukweli ni huu: mafanikio hayaji kwa sababu umeyataka. Yanakuja kwa sababu umekidhi vigezo vya kuyabeba.
Na vigezo hivyo havianzi nje. Havianzi kwenye pesa, kazi, cheo wala umaarufu. Vinaanzia ndani kabisa—kwenye utulivu wa nafsi na utayari wa kuitikia wito wako wa ndani.
Ndiyo maana kuna watu wamefanikiwa kwa nje lakini kwa ndani wanateseka. Wamepata kile walichotaka, lakini hawajapata kile walichohitaji.
Wamejenga maisha yanayoonekana, lakini hawakujenga nafsi inayoyaishi. Hawakutimiza hitaji la ndani, na hilo halifidiwi na chochote cha nje.
Maisha yanahitaji usawa. Mafanikio ya kweli hayazimi njaa moja huku yakileta njaa nyingine. Kuna watu wamefanikiwa kwenye kazi lakini wana njaa ya upendo; wamepoteza familia wakijenga taaluma.
Kuna waliofanikiwa kuwa maarufu lakini hawana rafiki hata mmoja wa kweli; wamezungukwa na kelele, si uaminifu.
Kuna waliofanikiwa kifedha lakini kwa sababu hawana utambuzi binafsi wamejaa kiburi, wanakosa hekima na staha ya kuishi na watu.
Hayo si mafanikio. Huo ni upungufu uliovaa jina la ushindi.
Nimeona vijana wengi sana wakitaka kufanikiwa. Wana ndoto, wana nguvu, wana bidii. Lakini hawana mizizi.
Wanapambana bila mwelekeo, wanajituma bila silaha sahihi. Hawana utambuzi binafsi.
Hawajajipanga ndani ya mafanikio wanayotafuta. Ndiyo maana wanachoka haraka, wanakata tamaa au wanabadilisha mwelekeo kila wakati.
Ukweli mchungu ni kwamba maisha yanahitaji mapambano. Lakini lazima utambue ni wapi upambane na utumie silaha gani.
Vinginevyo, unapambana kila siku lakini unasogea taratibu au hurudi nyuma bila kujua kwa nini.
Jina langu ni Mbulwa King’ung’e. Ninaendesha huduma za usimamizi wa maisha chini ya King Mentorship Program.
Na ni muhimu nieleweke mapema: hii si semina, si motivation, si maneno ya kukupa hamasa ya siku mbili. Hii si njia rahisi za kufanikiwa wala program ya kila mtu.
King Mentorship Program ni safari ya maisha. Ni safari ya kujengwa upya kwanza katika nafsi kabla hujajijenga kimaisha.
Ni kwa watu walio tayari kujiangalia kwa uaminifu, kujihoji bila kujitetea, kujikosoa bila kujidharau, na kujielewa kabla ya kutaka dunia iwape majibu.
Ni kwa watu wanaotaka kujua wao ni nani kabla hawajaanza kupambana na maisha.
Ni kwa watu wanaokubali kwamba chanzo cha matatizo mengi ya nje kiko ndani, na suluhisho la maisha thabiti nalo linaanzia ndani.
Kuna watu wachache tayari wamekubali ukweli huu. Wamekataa mafanikio ya haraka.
Wamekataa kuishi kwa kuiga maisha ya wengine. Wameamua kuanza na kazi ya ndani ili wajenge mizizi imara ya mafanikio ya nje.
Hao si wengi. Hawapigi kelele. Lakini wako tayari kulipa gharama ya kujijenga.
Sisemi wewe ni mmoja wao. Lakini kama umesoma mpaka hapa na ndani yako kuna sauti inayosema, “Nimechoka kukimbia bila kujielewa. Nataka kujijenga kwanza,” basi huu si ujumbe wa bahati mbaya kwako.
King Mentorship Program si kwa kila mtu. Lakini kama umefika mahali unajua kuwa mafanikio ya kweli hayawezi kujengwa juu ya nafsi usiyoifahamu, basi hatua inayofuata si kusoma zaidi—ni kuamua.
Uamuzi wa kuanza safari ya kujielewa. Uamuzi wa kujenga mizizi kabla ya matunda. Uamuzi wa kuacha kutafuta majibu nje wakati maswali yako yapo ndani.
Kama umefanya uamuzi huo, chukua hatua sasa. Wasiliana nami moja kwa moja. Hii si orodha ya kusubiri, wala si kundi la kujaribu. Ni safari ya watu walio tayari.
Huwezi kubadilisha maisha usiyoyafahamu.
Lakini ukijitambua, maisha hulazimika kubadilika.
Mimi ni Mbulwa King’ung’e.
Mwanzilishi, King Mentorship Program.
Mawasiliano: 0744 284 329
Comments
Post a Comment