Maisha Yako Yanaendeshwa na Nani?
Kabla hujaendelea, ni lazima niwe muwazi kabisa na wewe.
King Mentorship Program si kwa kila mtu. Si kwa mtu anayehitaji maneno ya kumfariji ili ajisikie vizuri kwa dakika chache.
Si kwa anayehitaji motisha ya kupandisha hisia halafu kesho arudi pale pale.
Wala si kwa anayehitaji mbinu za haraka za kupata pesa bila kujijenga ndani.
Hii ni kwa mtu aliyefika mahali anahisi kuna kitu ndani yake hakiko sawa.
Mtu anayeanza kuhoji maisha yake. Mtu aliyechoka kuishi kwa mazoea.
Kama bado unaamini kwamba mabadiliko ya kweli huja kwa kusikiliza hotuba nzuri tu, basi unaweza kuishia hapa.
Lakini kama kuna sauti ndani yako inayokuambia, *“Lazima pawe na zaidi ya haya ninayoishi sasa,”* basi endelea.
Kwa sababu hapa ndipo safari ya ndani inaanza.
Dunia inaendeshwa na maneno. Lakini si kila neno ni ukweli. Baadhi ni sumu iliyopakwa sukari.
Tangu utoto wako uliambiwa maneno. Uliitwa majina.
Ulipewa maelezo kuhusu wewe ni nani. Uliambiwa nini kinawezekana na nini hakiwezekani.
Uliambiwa nani unafanana naye, nani humpati, nani umemzidi.
Na polepole, bila hata kujua, maneno hayo yakaanza kuwa sehemu ya utambulisho wako.
Tatizo si kwamba watu walisema. Tatizo ni kwamba uliamini.
Ulizaliwa bila hofu. Lakini ulifundishwa uogope.
Ulizaliwa bila aibu. Lakini uliambiwa hustahili.
Ulizaliwa na uwezo. Lakini uliambiwa mpaka usome fani fulani, upate cheti fulani, ukubaliwe na fulani — huna thamani.
Kisaikolojia hali hii huitwa *hetero-suggestion* — wazo au pendekezo linalotoka kwa mtu mwingine na kuanza kuishi ndani yako kama ukweli.
Na ukishaliruhusu, fahamu yako ndogo haitaanza kulibishia. Italichukua kama amri. Na kuanza kulitekeleza.
Ndiyo maana mtu anaweza kuambiwa mara nyingi “wewe huwezi” mpaka anaacha kujaribu.
Anaweza kuambiwa “bila mimi hufiki popote” mpaka anaogopa kusimama peke yake.
Anaweza kuambiwa “mafanikio si ya watu kama nyinyi” mpaka anaanza kujiona mdogo hata mbele ya ndoto zake mwenyewe.
Na kila ulipokubali pendekezo hasi, hukubali tu neno — uliunda mipaka ndani ya akili yako.
Hebu jiulize kwa utulivu kabisa:
Ni imani zipi ulizonazo leo ambazo hukuwahi kuzikagua?
Ni hofu zipi unazoishi nazo ambazo hukuwahi kuzihoji?
Ni mipaka ipi umeweka juu ya uwezo wako ambayo si yako bali ulipewa?
Watu wengi wanaishi maisha ya kurithi.
Siyo urithi wa mali — urithi wa fikra. Urithi wa hofu. Urithi wa mitazamo. Urithi wa kujidharau.
Na kwa sababu hawajawahi kukaa chini na kuhoji, wanafikiri hiyo ndiyo “halisi.”
Sikiliza vizuri. Kila anayekuambia jambo, ana sababu nyuma ya pazia.
Wengine wanataka uogope.
Wengine wanataka uwategemee.
Wengine wanataka ubaki chini yao.
Wengine wanataka wakutumie.
Na kama hujitambui —utaitwa mfuasi, na utaishi hivyo milele.
Lakini bila kujali sababu zao, jukumu la kuchuja ni lako.
Mungu hakukupa akili kwa ajili ya kukariri kila unachosikia. Alikupa kwa ajili ya kuchanganua, kupima, na kuamua.
Lakini kuchanganua kunahitaji ujasiri. Kwa sababu mara nyingi utaanza kugundua kuwa mambo mengi uliyoyaamini si yako.
Na hapo ndipo safari ya kweli huanza.
Tatizo si pendekezo. Tatizo ni kuruhusu pendekezo liwe sehemu ya mfumo wako wa ndani.
Kwa sababu unapoamini, unaamuru fahamu yako ndogo itengeneze mazingira yanayothibitisha imani hiyo.
Ukijiamini hustahili, utaishi kama hustahili.
Ukijiamini huwezi, hutajaribu kwa nguvu zote.
Ukijiamini mafanikio ni magumu sana kwako, utaona kila kikwazo kama uthibitisho.
Siyo bahati mbaya.Ni imani iliyopandikizwa.
Ndiyo maana mabadiliko ya kweli hayawezi kuanzia nje.
Hayawezi kuanzia kwenye pesa. Hayawezi kuanzia kwenye nafasi. Hayawezi kuanzia kwenye mazingira. Lazima yaanzie kwenye mfumo wa fikra.
Na kubadilisha mfumo wa fikra si jambo jepesi.
Inahitaji uvunjaji. Inahitaji kukubali kuwa huenda umeishi kwa autopilot.
Inahitaji kukiri kuwa si kila ulichoamini kilikuwa chako.
Hii ndiyo kazi ya ndani. Na kazi ya ndani si ya kila mtu.
Kama umefika mpaka hapa, basi kuna kitu ndani yako kinajibu.
Kwa sababu mtu ambaye hako tayari kujitazama huwa anaacha kusoma mapema. Lakini wewe bado uko hapa.
Hiyo ina maana kuna mwamko unaanza.
Lakini tambua jambo moja muhimu sana —kusoma pekee hakubadilishi maisha. Maarifa bila maamuzi hubaki kuwa burudani ya akili.
Swali si umeelewa kiasi gani. Swali ni uko tayari kufanya nini baada ya kuelewa?
King Mentorship Program si mahali pa kukusanya maneno mazuri. Ni mahali pa kuvunja mifumo ya ndani na kujenga upya.
Ni safari ya kukuondoa kwenye utegemezi wa sauti za nje na kukupeleka kwenye uongozi wa ndani.
Na si kila mtu ana ujasiri wa safari hiyo.
Kama umechoka kuishi kwa imani ulizopewa, kama umechoka kuendeshwa na sauti zisizochujwa, kama uko tayari kujenga mizizi kabla ya kutafuta matunda —basi hatua inayofuata si kusoma zaidi.
Ni kuanza. Kwa uamuzi.
Mimi ni Mbulwa King’ung’e
Mwanzilishi — King Mentorship Program
📞 0744 284 329
Comments
Post a Comment