Sayansi ya Sala: Kwa Nini Wengi Wanaomba Lakini Wachache Wanapata..."
Mtazamo Rasmi wa King Mentorship Program
Kuna mambo ambayo hayawezi kubadilika maishani kwa sababu hatujayashughulikia kwenye mizizi yake.
Watu wengi wanasali. Wengi wanaomba. Wengi wanatamani.
Lakini wachache sana wanaelewa kanuni ya kujibiwa.
Katika King Mentorship Program hatufundishi maajabu ya hisia. Tunafundisha kanuni. Na kanuni hazibagui mtu, dini, dhehebu wala historia yako.
Na, kama kila sala ingekuwa inajibiwa kwa sababu ya hisia au ukubwa wa sauti, basi dunia hii isingekuwa na kilio.
Lakini bado kuna maombi mengi hayajageuka kuwa matokeo.
Kwa nini?
Kwa sababu sala si suala la dini kwanza.
Ni suala la mfumo.
Katika King Mentorship Program tumethibitisha jambo moja: Sala inayojibiwa ni ile inayofuata sayansi ya akili.
ELEWA HILI KWANZA
Ndani yako kuna mfumo wa ajabu.
Conscious mind – ndiyo lango.
Subconscious mind – ndiyo kiwanda.
Conscious inaamua nini kiingie.
Subconscious haitabishana — inachakata kile kilichoaminiwa.
Na hapa ndipo wengi wanaanguka. Unaomba kitu kimoja, Lakini unaona kitu kingine.
Ukisema unaomba mafanikio lakini ndani yako unaona umaskini, subconscious itachakata picha ya umaskini.
Ukisema unataka amani lakini ndani yako umejaa hofu, subconscious itazalisha hali zinazoendana na hofu.
Unasema unataka ndoa njema, lakini ndani unaamini “mapenzi ni maumivu”.
Hii ndiyo sababu sala nyingi hazijibiwi — si kwa sababu Mungu hasikii, bali kwa sababu hakuna upatanifu kati ya unachoomba na unachokiamini.
Katika KMP tunasema: Kile unachokiona ndani, ndicho kinachotokea nje.
Hivyo kama unaomba mafanikio lakini ndani unaamini wewe hustahili, subconscious haitachakata mafanikio — itachakata imani yako ya kutostahili.
Na kile inachochakata — ndicho kinachotokea.
MBINU 5 ZA SAYANSI YA SALA YA KWELI
1. Njia ya Kuona (Visualization yenye uthabiti)
Lazima ujione tayari ukiwa umepokea.
Siyo kwa dakika moja. Bali kwa uthabiti.
Kama ni biashara, jione ukiiongoza.
Kama ni afya, jione ukiwa mzima.
Kama ni ushindi wa kesi, jione tayari umefanikiwa.
Lazima ujione tayari umepokea.
Maisha yako ya sasa ni matokeo ya picha ulizoshikilia zamani.
Maisha yako ya kesho yatategemea picha unazoshikilia leo.
Hii si hadithi. Ni kanuni.
2. Njia ya Utulivu (Kupenya kwenye Subconscious)
Subconscious mind hufanya kazi vizuri wakati wa utulivu.
Ndiyo maana kabla ya kulala akili ya juu hupungua nguvu.
Huo ndiyo muda wa kupandikiza ombi.
Andaa sentensi fupi, yenye uhakika:
“Jambo hili limeisha.”
“Nimepokea.”
“Nimefanikiwa.”
Isikie kama tayari imetimia.
Irudie katika kuitamka mpaka ipokelewe na subconscios mind.
Hapa hatuchezi na maneno. Tunafanya kazi na mfumo wa akili.
3. Mbinu ya Kushukuru Kabla
Kushukuru kabla hujapokea ni tamko la umiliki wa ndani.
Unaposhukuru, unaitangazia subconscious kwamba jambo hilo tayari ni sehemu ya utambulisho wako.
Shukrani inalazimisha akili yako kutafuta uhalisia wa kile ulichoamini.
Hii ni kuunda hali ya ndani inayovuta matokeo ya nje.
Mfano:
Huna fedha lakini unasema: “Asante kwa utajiri unaokuja katika maisha yangu.”
Huna kazi lakini unasema: “Nashukuru kwa kazi nzuri niliyonayo.”
Huna biashara lakini unasema: “Asante kwa biashara inayokua kila siku."
Katika King Mentorship Program tunasisitiza: Shukrani ni ishara ya umiliki wa kiakili kabla ya umiliki wa kimwili.
4. Njia ya Kujitamkia
Maneno hubeba mwelekeo.
Unachojisemea mara kwa mara ndicho subconscious inachokubali kama ukweli.
Ukisema “mimi ni wa kushindwa” — subconscious haitapinga.
Ukisema “mimi ni mshindi” — haitapinga pia.
Hivyo usiruhusu kinywa chako kijenge gereza la maisha yako.
Usimalize sentensi hasi.
Usijitambulishe kwa matatizo.
Kusema ni kutengeneza mwelekeo.
5. Njia ya Kukemea
Kukemea ni kukataa kuiruhusu hali iwe utambulisho wako.
Ni msimamo wa ndani unaosema: “Hii si sehemu yangu.”
Unapokataa kwa uthabiti, unazuia kuipandikiza kwenye subconscious.
Na kile ambacho hakijapandikizwa, hakiwezi kuchakatwa.
Kwa ujumla huwezi kupata matokeo tofauti bila kuelewa mfumo.
Huwezi kuomba kwa hisia bila kanuni halafu utegemee kujibiwa.
Huwezi kubadili maisha bila kubadili picha, imani na lugha ya ndani.
Na kama hujui sayansi ya sala ya kweli —utaendelea kuomba bila kuona matokeo.
King Mentorship Program ipo kwa watu walio tayari kujifunza mfumo, si kuishi kwa mazoea.
Kwa sababu hapa tunafundisha kitu kimoja kikubwa: Dhibiti akili yako — au akili yako itadhibiti matokeo yako.
Na mtu anayejua kanuni, haombi kwa kubahatisha.
Anaomba kwa kuelewa.
Ndimi Mbulwa King'ung'e — Founder King Mentorship Program 👑
Mawasiliano:0744284329
Comments
Post a Comment