Tatizo siyo kinachosemwa, tatizo ni kukiamini na kukiruhusu kiwe SEHEMU ya MAISHA Yako...


Kabla hujaendelea kusoma, ni muhimu niwe muwazi KWAKO.

King Mentorship Program si kwa mtu anayehitaji mafanikio ya haraka, si kwa mtu anayehitaji motivation ya muda mfupi, wala si kwa anayehitaji mbinu za haraka za kupata pesa bila kujijenga ndani.

Kama unatafuta njia rahisi, majibu mepesi au matokeo ya haraka bila kazi ya ndani,
ni bora uishie hapa.

Lakini kama uko tayari kuanza na kujijenga katika nafsi yako kwanza kabla hujajijenga kimaisha, kama uko tayari kujihoji, kujikosoa na kuchukua uwajibikaji wa maisha yako, basi endelea — hapa ndipo safari yako inaanza.

Duniani TUNAISHI kwa maneno, lakini si kila kinachosemwa ni sahihi, mengine ni sumu ambayo inakuua huku ikikupa faraja.

Mungu alitupa midomo ili tusemezane, lakini siyo kusemezana tu tuongozane katika kuyaendea mema, lakini kama mema hayapo ni ngumu sana kuwa mwema na kuuishi wema. Ndiyo MAANA mikanganyiko duniani imekuwa mingi mbali na kuwa na wasemaji wengi.

Kwa sababu wengi wanasema wasivyovijua. Sasa unajifunza nini kwa msemaji ambaye hajui kwanini maisha yapo? Hajui kwanini yeye mwenyewe yupo.

Kinachotokea inakuwa ni kutoa shinikizo kwenye akili zako ili yeye akutumie.

Kisaikolojia hali hii hufahamika kama hetero suggestion kwa MAANA ya oni linalotokå kutoka kwa MTU mmoja Kwenda kwa MTU mwingine na endapo MTU anayeambiwa hivyo hatakuwa makini ataliruhusu pendekezo Hilo liendeshe maisha yake.

Kwa mfano ulizaliwa ukiwa safi, ukiwa na roho mpya ambayo haina uchafu wala rekodi lakini MTU Mmoja akasema umezaliwa ukiwa mchafu, ukiwa na laana, ukiwa na dhambi ya asili ili akugeuze Kiakili uwe mfuasi wake.

Mwingine anakuja na pendekezo hasi kuwa unaonekana unaumwa na watu wanakuwinda sana bila ulinzi nitakàkaokupa utafanyiwa vibaya Sana. 

Mwingine anakuambia YAANI wewé bila mimi huwezi kitu, hunà jeuri na huwezi kufika popote pale bila mimi akiwa na Lengo la kukutaka ubaki chini yake aendelee kunufaika na wewé.

Mwingine anakuambia kuwa kazi ni kila kitu ili uendelee kufanya kazi kwa sababu anajua ukielewa ukweli utafanya juhudi ili uache KAZI na yeye anataka ubaki KWAKE muda wote akufaidi maisha Yako yote.

Mwingine atakuambia huwezi kufanikiwa, huwezi kuelewa, mapenzi ni kwa ndege, utashindwa, huwezi, hustahili, hutafika popote pale ili aendelee kukuweka kwenye utegemezi.

Mwingine atakuambia kuwa huwezi kitu kama hujasoma wakati Watu waliishi wakiwa waelewa kabla ya hii mifumo ya Elimu inayotawala fikra za Watu kwa MAANA ya mitego ya kifikra.

Lakini kama nilivyosema hapo awali kuna wasemaji Sahihi na siyo Sahihi.

Na kila anayesema huwa anasukumwa na sababu iliyopo nyuma ya pazia ambayo ndiyo kiini cha yeye kusema.

Kwa hiyo kosa siyo pendekezo lililotolewa, kosa ni wewe unayeambiwa kutokuchuja na kuchanganua.

Mungû alikupa akili ili uitumie kuchanganua, kujikosaoa na kujisahahisha.

Hata Mimi hapa natoa suggestions KWAKO lakini akili yako ina uwezo mkubwa sana wa kuchanganua na kujua kwamba hiki ambacho King Mentorship Program anaandika kina maana.

Sasa kwanini usikilize kila jambo na ulikubali bila kuchanganua? Kwanini ujipeleke motoni.

Unafurahia TU kuitwa kondoo? Unafurahia kuitwa mtumwa asiye na faida? Unafurahia kuishishwa kimaskini?

Kosa ni lako. Hutaki kuchuja. Umefibuisha Sana akili zako.

Unapokubali pendekezo Fulani hasi maana yake unakuwa umelirhusu liwe SEHEMU ya maisha yako.

Na kwa sababu umeamini kitatokea KWAKO kama ulivyoamini au kuaminishwa visivyo sahihi.

Hivyo basi jifunze kukataa kila aina ya pendekezo hasi linalotolewa KWAKO.

Ukikataa MAANA hujaamini kitu hicho na Kama vile ambavyo huwa tunapokea kwa kadri ya imani zetu basi Hilo pendekezo hutaliruhusu litokee katika maisha yako kwa sababu umelikataa kiakili. 
 
Kama umefika mpaka hapa, kuna mambo mawili ni lazima yawe wazi.

La kwanza, umeona wazi kuwa King Mentorship Program si ya kila mtu.

Na la pili, kama bado unaendelea kusoma, ina maana kuna kitu ndani yako kimeshaamka.

Hii si safari ya kukupa majibu ya haraka.
Ni safari ya kukuuliza maswali ambayo hukuwahi kujipa nafasi ya kuyauliza.

Si kwa ajili ya kukufariji, bali kukujenga.
Si kwa ajili ya kukuchekesha, bali kukuweka sawa.

Lakini kama umefika mahali unajua kuwa huwezi tena kuendelea kuishi bila kujielewa, kama uko tayari kujenga mizizi kabla ya matunda, na kama uko tayari kubeba wajibu wa maisha yako bila kulaumu mazingira, basi hatua inayofuata si kusoma makala nyingine.

Hatua inayofuata ni kuwasiliana.

Si kwa kuuliza bei.
Si kwa kuomba maelezo marefu.
Bali kuthibitisha kuwa uko tayari kuanza safari ya ndani.

Mimi ni Mbulwa King’ung’e,
Mwanzilishi — King Mentorship Program.

📞 Mawasiliano: 0744 284 329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...