“Umefungwa na Hofu Bila Kujua? Jifunze Kuiondoa na Kuishi Wito Wako Bila Kizuizi...”


Hofu ipo. Na sote huwa tunahofia. Lakini si kila hofu uliyo nayo ni yako.

Wengi wetu tulikuzwa katika ulimwengu uliotengeneza mipaka: tukifundishwa kuamini kuwa hatuwezi, hatustahili, na ndoto zetu ni kubwa kuliko uwezo wetu.

Ulipokuwa mdogo, ulijaribu kufanya jambo fulani, ukaadhibiwa. Ukasema ukweli wako, ukakosolewa. Ukaonyesha uwezo, ukakosolewa kwa kushindwa. Na pale ulipokosea, wakakusema utaishia maskini, nyuma, au mdogo.

Polepole, ukajifunza kuishi kwenye mipaka hiyo, kujificha, kupoteza sauti yako ya ndani. Hukumu za wengine zikawa ukweli wako. 

Hofu ya kushindwa, kuchekwa, kutafsirika vibaya—hizo ndizo kamba zilizokuzuia kuangaza.

Bila hata wewe kujua, maisha yako, uhusiano wako, na uongozi wako wa maisha vilitegemea hofu ile iliyopandikizwa, si sauti yako.

Mimi nilijua hofu hiyo vizuri. Nilipoanza kuota wazo la King Mentorship Program, nilihofia:

Wataniitaje?

Nitachekwa?

Nitashindwa?

Lakini siku moja nikagundua: hofu hii haikuwa yangu. Ilikuwa programu iliyopandikizwa. Na programu inaweza kufutwa.

Polepole, nikaanza kuiondoa. Nikaanza kujenga sauti yangu ya ndani. Nikaanza kuamini uwezo wangu. Na nikagundua: hofu inaweza kuondolewa.

Sasa mimi si mtu mdogo. Sasa mimi ni MTU wa watu, nikiongoza wengine kuondoa hofu zao na kufanikisha ndoto zao.

Hofu haitabaki milele. Inaweza kufutwa. Inaweza kubadilishwa. Inaweza kuandikwa upya. 

Ni mpango uliopandikizwa unaoweza kuondolewa kwa ujasiri na hatua thabiti.

Hapa ndipo King Mentorship Program inapoingia. Tunasaidia watu kuvua vazi la hofu na kuvaa vazi jipya linaloendana na uhalisia wao.

Tunawasaidia:

Kurudisha sauti ya ndani.

Kuunda uthubutu

Kuishi wito wa ndani bila hofu

Ndugu, hauhitaji kubaki mdogo. Hauhitaji kuishi kwa kamba zisizoonekana. Hofu hukuzaliwa nayo na haina nafasi katika maisha yako sasa.

Safari ya uhuru, mamlaka yako ya ndani, na maisha yenye thamani inaanza na hatua moja: kuamua kuishinda hofu, kuwa MTU wa watu, na kuishi wito wako.

Ndimi, Mbulwa King’ung’e
Founder – King Mentorship Program
📞 0744 284 329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...