“Umepotezwa, Lakini Ukweli Upo Nao: Gundua Nafsi Yako Kabla Ya Kuiongoza Dunia...”
Maisha ni mwendelezo. Kila kizazi kinaendeleza kitu. Swali si kama utaendeleza, bali ni kama utaendeleza usahihi au upotevu?
Ukizaliwa kwenye familia isiyojua maana ya usahihi, huwezi kuujua. Ukikulia kwenye jamii isiyojitambua, ni vigumu kuwa sahihi. Ukisoma kwenye mfumo unaokupa taarifa za jana, utahitimu ukiwa umechelewa leo.
Hilo si kosa lako, lakini likibaki hivyo, litakuwa jukumu lako. Kuna kitu hakijawahi kufundishwa wazi: Unaweza kuishi maisha yako yote bila kujua wewe ni nani. Na hilo ndilo tatizo kubwa la kizazi hiki.
Mtoto anazaliwa akiwa safi. Ana vipaji, ana uwezo, ana ukubwa wake. Lakini anaanza kufundishwa mapema: “Usiulize sana. Usifikirie sana. Fanya kama wengine. Hivyo ndivyo tulivyozoea.”
Anapoingia shule, anapimwa kwa kukariri. Anapoingia kwenye jamii, anapimwa kwa kufanana. Anapoingia dini au mfumo, anapimwa kwa kutii. Hakuna anayemwambia: “Gundua wewe ni nani.”
Miaka 25 baadaye, huyo mtu ana kazi, majukumu, majina mengi, lakini hana majibu. Ndani yake kuna vita. Anapambana na hofu, mashaka, kujiona hafai. Lakini hajui chanzo. Hajui aliwahi kuwekewa mipaka ya kiakili kabla hajajijua.
Leo tunaishi kwenye dunia yenye mlipuko wa taarifa, zaidi ya wakati wowote katika historia ya ya uwepo wa viumbe watu.
Lakini kila anayekupa taarifa ana ajenda. Wengine wanataka uamini, wengine wanataka ufuate, wengine wanataka uogope, wengine wanataka uwe sehemu yao.
Taarifa nyingi hazijajengwa kukuuliza wewe ni nani. Zimejengwa kukutengeneza uwe wanavyotaka. Na ukiishi bila kujitambua, utaishia kuishi kwa kutumikia mifumo iliyokutengeneza.
Wengi tunaziishi vita za ndani. Tunataka mafanikio lakini hatujui kusudi. Tunataka thamani kubwa lakini hatujui thamani yetu. Tunataka kuongoza lakini hatujawahi kujiongoza.
Hatufundishwi kujua vipaji vyetu, hatufundishwi kuchunguza imani tulizopewa, hatufundishwi kuuliza: “Hii ninayoamini ni yangu au nilipewa?”
Tuliambiwa tu wadhaifu, tukaoneshwa makosa yasiyo yetu, tukaambiwa tu wakosefu, tukafundishwa kuogopa zaidi kuliko kufikiri.
Matokeo yake ni kwamba tunajiongoza kwa hoja ndogo, tunaongoza kwa mtazamo finyu, tunavaa utambulisho usio wa asili yetu.
Lakini ukweli haujawahi kufa. Ukweli unasubiri utambuliwe. Safari ya kuurudia huanza na hatua moja rahisi lakini ngumu: kuamua kujijua.
Sio kusoma zaidi, sio kufuata zaidi, bali kuanza kuhoji kwa ujasiri. Andika mambo matatu unayoamini kuhusu wewe, kisha jiulize: “Nilipewa au niligundua?”
Chunguza hofu zako kubwa: je, zina msingi wa uzoefu au zilirithishwa? Jiulize: “Kama nisingeogopa hukumu ya watu, ningekuwa nani?”
Ukishindwa kujibu haya kwa uhuru, ujue kuna sehemu yako bado imefungwa. Hapo ndipo uongozi wa nafsi huanza.
Hapa hatujengi wafuasi. Tunajenga viongozi wa nafsi zao. Hapa hatukuambii uamini, tunakuongoza kugundua.
Hapa hurudishwi kwenye mfumo, unarudishwa kwenye uhalisia wako. Tunagusa mizizi ya utambulisho, tunafungua fikra, tunajenga misingi ya kuishi kwa ufahamu.
Kwa sababu huwezi kuongoza dunia kama hujaweza kuiongoza nafsi yako, na huwezi kuiongoza nafsi yako kama hujawahi kufundishwa wewe ni nani.
Kama umefika hapa na kuna kitu ndani yako kimeguswa, usiipuuze sauti hiyo. Hiyo si bahati, ni mwamko. Chukua hatua. Njia moja rahisi ya kuanza ni kuwasiliana nasi.
Pata mwongozo, pata mentorship, pata uelewa wa kweli. Uko tayari kuishi kwa uhalisia, kuongoza nafsi yako, na kugundua vipaji vyako.
📞 0744 284 329
Mbulwa King'ung’e - Founder, King Mentorship Program
Comments
Post a Comment