“Unayaongoza Maisha Yako au Yanakuongoza?”*
Kuna aina mbili za watu duniani. Wale wanaoishi kwa matukio, na wale wanaoongoza maisha yao.
Wale wanaoishi kwa matukio huacha kila kitu kiwe bahati. Hawa wanaamka asubuhi bila malengo ya kweli, wakienda kazini bila kufikiria kesho, na kuishia kufanya kile ambacho wengine wanasema ni sahihi.
Lakini wale wanaoongoza maisha yao wanajua wanakoenda. Kila hatua ya leo ina maana kwa kesho yao. Kila uamuzi ni sehemu ya ramani ya maisha yao.
Ukweli ni kwamba kila mtu ni kiongozi. Lakini si kila mtu ni kiongozi sahihi.
Kwa nini? Kwa sababu kiongozi wa kweli huongozwa na maono.
Kiongozi kipofu si mtu asiye na uwezo. Mara nyingi ni mtu mwenye bidii sana. Anafanya kazi, anajituma, ana ndoto nyingi.
Lakini ukimuuliza swali rahisi tu, “Unajiona wapi baada ya miaka mitano?” anakupa jibu la jumla, au anakaa kimya.
Na hapo ndipo tatizo linaanzia.
Kwa sababu mtu asiyeona mwisho wake, hawezi kupanga mwanzo wake kwa usahihi.
Maono si ndoto za mchana. Maono ni picha kamili ya maisha unayotaka kuyaishi. Ni kuona familia yako kabla haijawa. Ni kuona hali yako ya kifedha kabla haijaimarika. Ni kuona thamani yako kabla haijajengwa. Ni kuona mchango wako kabla haujaonekana.
Ukishajipa muda wa kukaa chini na kujiuliza, “Nataka maisha yangu yaweje kweli?” unakuwa umeanza kuongoza.
Watu wengi hawafanyi kosa kwa sababu ni wabaya. Wanafanya makosa kwa sababu hawajachagua mwelekeo.
Wanaingia kwenye mahusiano bila kujiuliza wanataka maisha ya aina gani. Wanachagua kazi bila kujiuliza wanataka kuwa watu wa aina gani. Wanakubali kila fursa kwa sababu hawajui ipi inaendana na kesho yao.
Lakini mtu ambaye tayari ameiona kesho yake huwa na utulivu wa ajabu. Hachukui kila nafasi. Hafuati kila ushauri. Hakubali kila mwaliko. Siyo kwa sababu ana kiburi — bali kwa sababu ana ramani.
Na ramani hubadilisha maamuzi.
Unapoanza kuona kesho yako kwa uwazi, unaanza kujipima. Unaangalia maisha yako ya sasa na kujiuliza kwa uaminifu: “Hiki ninachokiishi leo kinanifikisha kule ninapotaka kufika?”
Ukigundua kuna vitu vinakupeleka mbali na mwelekeo wako, hapo ndipo uongozi wa kweli unaanza. Unaacha kulaumu. Unaacha kuishi kwa mazoea. Unaamua.
Wakati mwingine uamuzi huo unamaanisha kuacha mazingira fulani. Wakati mwingine ni kubadili tabia. Wakati mwingine ni kukubali kuwa umeishi chini ya uwezo wako kwa muda mrefu.
Lakini huwezi kufanya mabadiliko hayo kama hujaona kwanza picha ya maisha unayotaka.
Jaribu kufanya jambo moja leo. Tulia dakika chache bila simu, bila kelele. Jiulize kwa kina: kama nitaendelea kuishi hivi nilivyo sasa kwa miaka mitano ijayo, nitafurahia maisha hayo?
Usijidanganye. Jibu kwa ukweli. Halafu jiulize tena: maisha ninayotamani kweli yakoje? Tofauti kati ya majibu hayo mawili ndiyo umbali kati ya ulipo na unapopaswa kuwa.
Uongozi wa kweli hauanzi kwa kuongoza watu. Unaaanza kwa kuongoza nafsi.
Na mtu anayejua anakoenda hahitaji kusukumwa kila siku. Anahitaji taarifa sahihi, mwanga sahihi, na mazingira sahihi yatakayomsaidia kufika huko.
Ndiyo maana katika King Mentorship Program hatuanzi kwa kukupa mbinu za mafanikio.
Tunaanza kwa kurekebisha mtazamo. Kwa sababu mbinu bila maono ni harakati bila mwelekeo. Unaweza kukimbia sana, lakini bado usifike popote.
Kuwa kiongozi si cheo. Si jina. Ni jukumu la kuchagua unakopeleka maisha yako.
Swali si kama wewe ni kiongozi. Swali ni moja tu — unayaongoza maisha yako, au yanakuongoza?
Na ukishajibu hilo kwa uaminifu, safari yako inaanza hapo.
Lakini ukweli mmoja lazima ueleweke.
Watu wengi wanafika hatua ya kutambua kuwa wamekuwa wakiishi bila mwelekeo… halafu wanaishia hapo hapo. Wanatambua, wanaguswa, wanahamasika kidogo — kisha maisha yanaendelea kama kawaida.
Kwa sababu kutambua pekee haitoshi.Unahitaji mfumo. Unahitaji mwongozo. Unahitaji mtu atakayekuongoza bila kukubembeleza.
Kama umesoma mpaka hapa na kuna kitu ndani yako kimegongwa — hiyo si bahati. Ni ishara.
Ishara kwamba umefika mahali huwezi tena kuendelea kuishi kwa mazoea.
Ishara kwamba unahitaji zaidi ya motisha.
Unahitaji mwelekeo.
Na kama uko tayari kujenga mizizi kabla ya kutafuta matunda, kama uko tayari kubeba jukumu la maisha yako bila kulaumu mazingira, basi hatua inayofuata si kusoma makala nyingine.
Hatua inayofuata ni kuwasiliana.
Si kwa kuuliza bei. Si kwa kutafuta maelezo marefu. Bali kuthibitisha kuwa uko tayari kuanza safari ya ndani.
Mimi ni Mbulwa King’ung’e,
Mwanzilishi — King Mentorship Program.
📞 0744 284 329
Comments
Post a Comment