UKWELI MCHUNGU: UNAISHI KULINDA IMAGE, SIYO MAISHA YAKO…
Watu wanakuona kama umefika — kwa kutumia vigezo vya nje.
Wanakuita boss. Kiongozi. Tajiri. Bwana mkubwa.
Wanakusalimia kwa adabu. Wanakutazama kama mfano wa mafanikio.
Na wewe… umezoea hilo jina, mpaka umesahau wewe ni nani bila hilo.
Lakini kuna ukweli ambao hujawahi kukubali — hata ukiwa peke yako usiku:
Hii image unayoivaa… siyo mafanikio.
Ni kifungo.
Kwa sababu kila uamuzi unaotaka kufanya,
lazima uupitishe kwanza kwenye hofu moja:
"Watu watasemaje?""Watanionaje?" "Watanifikiriaje?"
Sina maana ya kupuuza watu — lakini ukweli ni huu: ukishindwa kuchagua watu sahihi wa kubaki nao, utaishia kuishi maisha ya kuwaridhisha wote… na kupoteza wewe mwenyewe.
Unataka kubadilika… lakini unaogopa utaonekana umeanguka.
Unataka kuanza upya… lakini unaogopa kupoteza thamani ya uongo uliyojenga — au uliyojengewa na mfumo.
Kwa hiyo unaendelea.
Unaamka kila siku ukiigiza maisha.
Unaongea maneno ambayo siyo yako.
Unacheka tabasamu ambalo halikutoki moyoni.
Na watu wanakushangilia…
wakati wewe unajichukia kimya kimya.
Kila siku unapoteza sehemu ya nafsi yako,
ili kulinda sura ambayo siyo wewe.
Na taratibu… unakuwa mgeni ndani ya maisha yako mwenyewe.
Hapa ndipo vita ya ndani inaanza.
Mtu wa NDANI anataka kuishi.
Mtu wa NJE anataka kuonekana anaishi.
Mimi nilipitia hii hali mwaka 2020.
Baada ya kumaliza safari ya mfumo wa ELIMU, nilikaa chini nikajifanyia tathmini…
Nikagundua kitu kimoja cha kutisha:
Nilikuwa sina kitu ndani. Nilikuwa mtupu.
Ndipo nikafanya maamuzi magumu:
Nikaanza kumpuuza mtu wa nje aliyetengenezwa na mifumo…
na kuanza kumjenga mtu wa ndani — ambaye ndiye mimi halisi.
Haikuwa rahisi.
Nilihangaika. Nilipambana. Nilijivunja… na kujijenga upya.
Na leo ninapokuandikia haya — nimevuka kiwango kile nilichokuwa nakihofia.
Ndiyo maana King Mentorship Program haipo kwa ajili ya motisha ya muda mfupi.
Ipo kwa ajili ya kumuamsha mtu wa NDANI —
kwa kumpa maswali sahihi yatakayomrudisha kwenye ukweli wake.
Ukweli mchungu ni huu: Haujapenda mafanikio yako… umeogopa kuyaacha.
Na hapo ndipo tofauti ya mtu huru na mtumwa ilipo:
Mtu huru anaweza kupoteza kila kitu — lakini hawezi kujipoteza.
Mtumwa?
Analinda kila kitu… mpaka anajipoteza kabisa.
Sasa acha kujidanganya.
Jiulize hili kwa uaminifu wa kikatili: Kama kesho ungeamka bila hii image uliyoijenga…
Je, bado ungejua wewe ni nani?
Au ndiyo ungegundua…
maisha yako yote ulikuwa unaigiza?
Ndimi Mbulwa King’ung’e
Founder — King Mentorship Program
📞 Mawasiliano: 0744 284 329
Comments
Post a Comment