MWANAMKE, MAISHA YAKO HAYAJAHARIBIKA — UMEENDESHWA TU NA MSUKUMO WA NJE

Mwanamke wa Kitanzania, nahitaji niseme na wewe moja kwa moja kupitia ujumbe huu, kwa sababu huenda maisha yako leo yamejaa maswali mengi kuliko majibu.

Huenda umefika mahali unajiuliza kimya kimya, “Hivi maisha yangu yaliharibika wapi?”

Unaangalia nyuma unaona maamuzi uliyofanya, unaangalia mbele unaona hofu ya kesho, na katikati unajikuta ukijilaumu kana kwamba wewe ndiye uliyesababisha kila kitu.

Lakini ukweli ambao wanawake wengi hawajawahi kuambiwa ni huu: wanawake wengi hawaharibu maisha yao kwa sababu ni wabaya au dhaifu, wanaharibu maisha yao kwa sababu wameendeshwa na msukumo wa nje tangu wakiwa wadogo bila kujitambua.

Wanawake wengi wamelelewa katika mazingira yenye makatazo mengi kuliko maelekezo.

Uliambiwa sana usifanye hivi, usionekane vile, usifanye makosa, usiharibu maisha yako, lakini hukufundishwa jinsi ya kujitambua au kufanya maamuzi sahihi.

Uliambiwa sana kuogopa, lakini hukufundishwa kuelewa. Kadri ulivyokua, hofu ulizojengewa zilianza kuwa sehemu ya maisha yako.

Ulianza kufanya maamuzi si kwa sababu unajua unataka nini, bali kwa sababu unaogopa watu watasema nini.

Hofu hiyo ilianza kukuongoza katika mahusiano, katika maamuzi ya maisha, na hata katika ndoto zako.

Kuna mwanamke mmoja aliyeshiriki kwenye program za utambuzi binafsi chini ya King Mentorship Program, ambaye hadithi yake imewasaidia wanawake wengi kujiona ndani yake.

Alilelewa katika familia ya dini na maadili, lakini pamoja na maadili hayo kulikuwa na makatazo mengi sana bila kuelekezwa kwa vitendo.

Aliogopeshwa sana kuhusu mahusiano na mimba, hadi akajikuta anakua akiwa na hofu kubwa kuhusu maisha ya mahusiano.

Kadri miaka ilivyokwenda, presha zilianza kuongezeka kutoka kwa ndugu na jamii. 

Maneno kama: “ukifika miaka 28 hujaolewa basi umechelewa” yalianza kumjenga hofu ya kufanya maamuzi kwa haraka.

Kutokana na hofu hiyo na kukosa maarifa ya kujitambua, aliingia kwenye mahusiano bila kuchunguza kwa kina.

Hakujua kuuliza maswali sahihi, hakujua namna ya kumwelewa mwanaume, na hakujua namna ya kujilinda kihisia.

Anasema: “Nilijikuta nikiwa na hofu kubwa kuhusu mahusiano. Kwa sababu ya kukosa maarifa ya kuchunguza mwenza, niliingia kwenye mahusiano bila kuelewa ninachofanya, na hatimaye nikajikuta kuwa single mother.”

Aliishi maisha ya kujilaumu, maisha ya hofu kuhusu kesho, na maisha ya kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Kila siku alihisi kama maisha yake yameharibika na hakuna njia ya kurudi nyuma.

Lakini mabadiliko yalianza pale alipogundua kuwa hakuwa peke yake.

Alianza kuona kuwa wanawake wengi wanapitia hali kama yake, na wengi hawajui nini cha kufanya.

Ndipo akaamua kuanza safari ya kujitambua kwa kujiunga na *King Mentorship Program.

Katika miezi ya kwanza alianza kuelewa historia yake mwenyewe na kuona jinsi malezi yake yalivyomjengea hofu.

Alianza kuelewa kuwa maneno aliyosikia tangu utotoni yalikuwa yanaendesha maamuzi yake bila yeye kujua.

Kadri alivyoendelea, alianza kuondoa hofu zilizokuwa zimejengwa ndani yake kwa miaka mingi.

Alianza kuelewa kuwa kubezwa si mwisho wa maisha, na kwamba thamani ya mwanamke haitokani na maoni ya watu bali na uelewa wake mwenyewe.

Polepole alianza kujenga maamuzi mapya yaliyotokana na uelewa badala ya hofu.

Ndipo alipoweza kusema: “Sasa ninaanza kuona kuwa tatizo halikuwa mimi, bali kukosa maarifa sahihi.”

Na sentensi hii ikawa mwanzo wa maisha mapya kwake.

Mwanamke, kama unasoma ujumbe huu na unahisi moyo wako unaguswa, huenda hii si bahati.

Huenda wewe pia umeishi maisha yanayoendeshwa na presha za nje, maneno ya watu, au hofu za zamani.

Huenda umefanya maamuzi ambayo leo yanakufanya ujilaumu kimya kimya.

Lakini nataka ujue jambo moja muhimu sana:

Maisha yako hayajaisha. Hayajaharibika — umeendeshwa tu na msukumo wa nje bila kujitambua.

Na siku utakapoanza kujitambua, ndipo utakapoanza kuishi maisha yako halisi.

Ndani ya King Mentorship Program, kuna program maalumu za utambuzi binafsi za miezi mitatu zinazowasaidia wanawake kuelewa historia zao, kuondoa hofu, na kujenga maamuzi sahihi ya maisha yao.

Hii si safari ya siku moja, bali ni safari ya kujijenga hatua kwa hatua.

Kama umejisikia kuguswa na ujumbe huu, usipuuze hisia unazozipata sasa.

Huenda huu ndio mwanzo wa mabadiliko yako.

Kwa sababu mwanamke anayejitambua haogopi maisha, haogopi kuanza upya, na haogopi kubezwa.

Anaanza kuishi kwa uelewa badala ya hofu.

Kama mwanamke mwenzako aliweza kuanza upya baada ya kuanguka, basi na wewe unaweza kuanza safari yako ya kujitambua leo.

📩 Kwa maelezo zaidi au kuanza safari yako:
WhatsApp: 0744 284 329

Ndimi: Mbulwa King'ung'e
Founder, King Mentorship Program.

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...