UTU ULIPOTEA WAPI? SIRI YA MGAWANYIKO WA WATU..." Makala ya kuamsha fikra kuhusu chanzo cha migawanyiko ya WATU, imani, lugha na uelewa wa maisha...

Kuna baadhi ya vitu vimezoeleka na vinachukuliwa kama vya kawaida sana katika maisha yetu, lakini kwa uhalisia ni chanzo kikubwa cha kukosekana kwa undugu wa kweli, upendo na umoja wa kiutu.

Ni kweli kabisa kwamba mambo ya kiimani ya mtu hayakuhusu mwingine moja kwa moja. Hata mimi nakiri hilo.

Lakini swali linakuwa: kama anayeabudiwa ni Mungu mmoja, anaelezwaje katika imani mbalimbali kuhusu mgawanyiko na tofauti zinazotokea kati ya wanaomuabudu, hasa pale ambapo imani hizo zinatofautiana na kugongana katika hoja na taratibu?

Bila shaka umeshawahi kuona ambacho hutokea katika familia ambayo baba na mama hawana umoja. Huwepo wafuasi wa baba na wafuasi wa mama.

Wafuasi hao mara nyingi hawapatani; upande mmoja haumkubali mwingine, licha ya wote kutoka kwenye chanzo kimoja—yaani uzao wa baba na mama.

Hali hii imejirudia pia miongoni mwetu sisi watu. Tumegeuzwa kuwa mashabiki wa makundi fulani, huku tukipuuza mengine. Tunajiona sisi ndio sahihi, na wengine hawako sahihi.

Hatufundishwi kwa undani kuhusu mfumo na utaratibu sahihi wa kuishi hapa duniani. 

Hatuelekezwi jinsi ya kuishi kwa namna inayolinda miili yetu na utu wetu. Badala yake, mara nyingi tunapandikizwa migawanyiko na uadui.

Tunaambiwa tunatoka kwenye chanzo kimoja, na hilo linaonekana kukubalika. Lakini hatuambiwi chanzo hicho cha utu wetu kilikuwa kinaishi kwa taratibu zipi. 

Hatuambiwi kilikuwa na rangi ipi, au kama mgawanyiko wa rangi ulitokana na nini. Hatuambiwi lugha yake ilikuwa ipi, wala namna ya mawasiliano yake na Muumba yalifanyika kwa lugha IPI...

Tuna imani tofauti, lakini hatujui kama mtu wa kwanza alikuwa na imani ipi kati ya hizi zilizopo leo. 

Tuna makabila, lakini hatujiulizi yeye alikuwa kabila gani. Tuna majina ya ukoo, lakini hatujui chanzo chake kilikuwa nini.

Tumeenea duniani kote katika mabara yote saba, lakini hatuelewi kwa kina namna usambaaji huo ulivyotokea. Tuko hapa kana kwamba tulitokea bila mpangilio wa kueleweka.

Tumejifunza elimu kutoka kwa viumbe wa ulimwengu, wakiwemo majini na malaika, lakini hatuelewi elimu yetu ya kuishi hapa duniani ilianza vipi. Kila kitu kimekuwa kama fumbo.

Swali linabaki: ni kwa nini tuumbwe na kisha tufumbwe ilhali hatujui ukweli kamili wa maisha? Je, tunatafuta ukweli kwa vyanzo ambavyo navyo havina ukweli kamili?

Kwa mtazamo huu, inaonekana kama lengo ni kuvurugana kama ilivyo sasa. Inaonekana lengo ni kuharibiana kimaisha kama ilivyo sasa. Hapo ndipo mtu anajiuliza: tusemeje?

Hakuna anayejua ukweli wote, lakini kila mmoja anajaribu kuuliza na kutafuta.

Tuna siku za kuabudu zilizopangwa, lakini hakuna anayejiuliza kwa kina kama chanzo cha imani hizi ni kimoja, na kama ni kimoja, kwa nini taratibu zake zinatofautiana sana.

Kwa uelewa wangu, kila kundi lina Mungu wake, na Mungu wa kundi moja si sawa na wa kundi jingine—ndiyo maana migongano imeendelea kuwepo.

Ndiyo maana kila sehemu ukiwepo, unaambiwa ujilinde na manabii wa uongo. Kila mmoja anawaona wengine kuwa wa uongo. 

Hapo ndipo swali linazidi kuwa kubwa: ni nani wa kweli kama kila mmoja anamkataa mwingine?

Hali hii inaleta mkanganyiko wa fikra, hasa kama kuna utabiri wa uwepo wa watu hawa. 

Kama walitabiriwa, ina maana mtabiri naye ana nafasi katika mnyororo huu wa changamoto za kiimani.

Bila utabiri huo, haya yangetokea? Swali linabaki wazi.

Hakuna uelewa tofauti hapa duniani. Uelewa ni kiwango cha juu cha kuelewa uwepo uliofanya vinavyoishi na visivyoishi kwa namna moja—kuyaelewa maisha kuanzia yalianzaje, na kipi hutokea baada ya kifo.

Kila tofauti ndogo ndogo tunazoziona duniani ni matokeo ya kupishana katika ujuzi, ufahamu na utambuzi, si Tofauti ya uelewa. Hatuwezi kutofautiana uelewa. 

Kwa sababu katika uelewa wa juu, watu wanapofikia kiwango hicho, hupunguza mgongano wa fikra na kubaki katika kutafakari zaidi kuliko kupingana.

Na hilo ndilo lengo la Mungu kufanya maisha—alitaka kiumbe kiwe kielewa, kimjue Mungu, kiyajue maisha, halafu kijue taratibu za kuishi.

Lakini swali ni moja: wewe ni muelewa?

Anyways, nitoe uchanganuzi mfupi kabla sijafunga mjadala huu.

HAKUNA Mungu wa kabila fulani. HAKUNA Mungu wa taifa fulani. HAKUNA Mungu wa asili fulani. HAKUNA Mungu wa bara fulani. HAKUNA Mungu wa dini fulani. Hayupo Mungu wa eneo fulani.

Ila kuna Mungu mwenye vyote hivi—aliyefanya vinavyoishi na visivyoishi.

Na kama hujui, hifadhi ya jina Mungu ilihifadhiwa na mtu wa kwanza kuumbwa na mambo ya Mungu.

Jina hili alifundishwa mtu wa kwanza na muujiza wa Mungu. Alianza kuambiwa kwamba yeye ni mtu—hata jina “mtu” halikuwepo kabla hajaumbwa. 

Na hata jina “Mungu” kabla ya uumbaji halikuwepo. Ulikuwa ni uwepo tu uliofahamika kama “vradiens kimmiad kwa kibantu”.

Kwa hiyo jina Mungu linatokana na lugha ya kiutu, yaani Kibantu “munu hungu” (Mungu) kwa maana ya mwenye vyote.

Jina hili Mungu lilisambaa katika mabara yote saba kwa sababu mtu wa kwanza alikuwa na agano la kuzaa katika mabara yote saba.

Hivyo nukuu ya chanzo cha kiutu inatambua kuwa jina Mungu ni moja tu, halina tafsiri—lipo kama lilivyo kwa sababu ndilo lililokuwepo kwenye dunia hii.

Ninyi watu mlikuwa na maandishi yenu ya Kibantu. Hiyo ndiyo lugha yenu, tena kwa mabara yote saba—je mnaijua? Mnajua herufi zake?

Kumbe mlivurugwa kidogo sana kwenye lugha, na kwa kuwa lugha ndiyo huleta uchanganuzi wa kweli, mkivurugwa kwenye lugha mtawezaje kuwa waelewa?

Matokeo yake, kila kilichoabudiwa katika eneo fulani, kwa kukosa uelewa wa maana yake halisi, mkakiita Mungu ilhali kinaonekana wazi kabisa kuwa ni kiumbe chenzenu.

Mfano, kwa Wanyakyusa kulikuwepo dhana ya Kyala aliyekuwa anaabudiwa kwa mfumo wao wa kiimani. 

Lakini baada ya mzungu kuingia kipindi cha ukoloni na kuleta simulizi zake za kiimani, yule Kyala akaanza kufananishwa na Mungu wa kikoloni.

Hapo ndipo vurugu kubwa ya kiutambuzi ilipoanzia. Watu wakaanza kuchanganya chanzo cha asili cha imani zao na tafsiri mpya walizoletwa nazo wageni.

Wakaona Mungu ni kama kitu unachoweza kukiunda mwenyewe kutokana na imani yako. Yaani hata jiwe linaweza kuwa Mungu kwako kwa sababu lilifanywa na Mungu na umeamini hivyo. 

Lakini wasijue kwamba Mungu ni uwepo mkuu usiochangamana na vinavyoishi, wala kugeuzwa na mawazo ya viumbe.

Taratibu, kizazi kikaanza kurithi majina bila kujua maana zake za awali, kikaabudu kwa mazoea bila kuelewa chanzo chake.

Ndiyo maana leo hii watu wengi wanarithi dini, lakini hawarithi uelewa wa kwanini wanaamini wanachoamini.

Swali KWAKO, Mungu ni Nini?

Nimemaliza. Naitwa Mbulwa King’ung’e, mwalimu wa maisha na mambo ya Mungu.

SENDE ESUPRIY DEWO OCHI 

Mawasiliano: 0744284329

Comments

Popular posts from this blog

Kusudi, Njaa na Ajira: Msingi wa Mageuzi ya Elimu ya Kiafrika

Taifa Lililopewa Uhuru wa Mwili, Lakini Limetekwa Kiakili...

Je, Unataka Kujua Chanzo Cha Matatizo Mengi Yanayozikumba Jamii Nyingi Za Kiafrika? Kama Jibu Lako Ni Ndiyo Soma Hii...