Wazo Moja Linaweza Kubadilisha Maisha ya Maelfu...
Kuna wakati unafika katika maisha ambapo unagundua kwamba tofauti kati ya mtu anayebadilisha dunia na yule anayebaki kuwa mtazamaji siyo pesa. Siyo mazingira. Wala siyo bahati. Tofauti kubwa inaanza kwenye wazo.
Leo asubuhi nilikuwa nasoma Think and Grow Rich, hasa sura inayozungumzia *Imagination*.
Kadri nilivyozama ndani ya kurasa zake, nilikutana na simulizi kuhusu wazo lililogeuka kuwa moja ya bidhaa maarufu zaidi duniani — Coca-Cola.
Baadaye nilipofika hotelini na kuagiza kinywaji hicho, nilikishika kwa mtazamo tofauti kabisa. Sikukiona tena kama soda tu. Niliona nguvu ya wazo la Mtu mwenzangu.
Nikaanza kujiuliza: ni watu wangapi leo wanapata ajira kupitia wazo hilo moja?
Ni familia ngapi zinaishi kupitia kampuni hiyo?
Ni wauzaji wangapi, wasambazaji, madereva, wabunifu, marketers, waandishi wa matangazo na wafanyakazi wengine ambao maisha yao yameguswa na mtu mmoja aliyethubutu kuamini wazo lake?
Hapo ndipo nilipozidi kuelewa kwamba kila Mtu amepewa kitu cha aina yake ndani yake.
Kila mmoja wetu ana wazo ambalo linaweza kuwa suluhisho kwa watu wengine. Wazo ambalo linaweza kuwa chanzo cha ajira. Chanzo cha mabadiliko. Chanzo cha matumaini.
Tatizo ni kwamba watu wengi huzika mawazo yao kabla hayajapata nafasi ya kuishi.
Wengine huogopa kuanza.
Wengine husubiri mazingira yakamilike.
Wengine huamini hawana uwezo.
Na wengine huamini kwamba mafanikio ni ya watu wachache waliozaliwa na bahati.
Lakini ukweli ni huu: dunia hubadilishwa na watu wanaothubutu kuanza na kile walichonacho.
Mimi mwenyewe kupitia wazo la kuanzisha programs za utambuzi binafsi, nimeona maisha ya watu yakibadilika.
Nimeona watu wakijitambua upya. Wengine wakipata ujasiri wa kuanza biashara. Wengine wakijifunza kujisimamia. Wengine wakitoka kwenye hali ya kukata tamaa na kuanza kuona thamani yao.
Wengine wakianza kujiajiri na kufikiri kuajiri wengine...
Na hapo ndipo maono yangu yalipozidi kuwa makubwa zaidi.
Wazo langu siyo kufundisha tu.
Wazo langu ni kujenga kizazi kinachojielewa.
Kizazi kinachoweza kujisimamia.
Kizazi kinachoweza kujiongoza.
Kizazi kinachoweza kutumia mawazo yake kuleta thamani duniani.
Nimejizatiti kutoa huduma bora za usimamizi na utambuzi binafsi. Nimejizatiti kufundisha watu kuhusu maisha, uongozi binafsi, fikra, maamuzi na namna ya kuishi kwa kusudi.
Kwa sababu naamini kabisa kwamba Mtu akijitambua vizuri, anaweza kubadilisha maisha yake — na akibadilisha maisha yake, anaweza kubadilisha ulimwengu unaomzunguka.
Kwa hiyo leo nataka kukuuliza swali moja tu:
Je, wazo lako linaweza kubadilisha nini duniani?
Usidharau kile kilichopo ndani yako. Huenda jambo ambalo unaliona ni dogo leo, kesho likawa sababu ya watu wengi kupata ajira, matumaini na maisha bora.
Anza na wazo.
Liamini.
Lipe muda.
Lifanyie kazi.
Na dunia itaanza kuona thamani iliyokuwa imejificha ndani yako.
Karibu kwenye programs zangu za utambuzi binafsi chini ya King Mership Program.
Ninaitwa Mbulwa Kingunge.
📞 Mawasiliano: 0744284329
Comments
Post a Comment